Friday 22 December 2017

UFAHAMU UGONJWA WA KUOZA VITAKO(BLOSSOM END ROT) KWA MATIKITI NA NYANYA.

Kwanza tujue kuwa ugonjwa huo unaitwa blossom end rot na hausababishwi na wadudu bali ni matokeo ya ukosefu wa madini ya calcium kwa mimea pindi matunda yanapoanza kubebwa kwenye shina.
sababu za ukosefu/upungufu ni:-

1.kutokuwepo kwa mpangilio sahihi wa umwagiliaji.
Hii ni pale unakuwa unamwagilia bila mpangilio mfano asubuhi mara mchana,wiki moja mara wiki mbili n.k.
2.pH ya udongo.
Ili madini haya ya calcium yawepo na kuweza kuchukuliwa na mmea ni lazima udongo uwe na pH kati ya 6-6.7,inapotokea udongo umefikia pH ya 5.5 kushuka ndipo hata kama utaweka vipi mbolea ya calcium inakuwa bure kabisa kwa kuwa mbolea (Ca ions) itashikiliwa kwenye udongo na haitaweza kuchukuliwa na kutumiwa na mmea.Hapo ndipo ardhi inahitaji kuwekwa lime ili iweze kurudia hali yake.
3.Kiwango kikubwa cha matumizi ya mbolea za nitrogen huweza kukuza majani kuwa makubwa na hivyo kufanya virutubisho vya calcium kuelekezwa kwenye mmea(majani) zaidi kuliko kwenye tunda na hivyo kupelekea seli zilizochini na mwisho wa tunda kuanza kufa na hatimae tunda lote kuwa halina maana.
4.Kuna wakati matumizi ya mbolea zenye jamii ya ammonium huweza kuzibana calcium ions kwenye udongo zisipatikane na kutumiwa na mmea.Hivyo kuwa makini na mbolea unazotumia kwenye shamba lako.
MAPENDEKEZO.
1.Uwe na muda wa umwagiliaji wenye mpangilio.
2.Kapime udongo wako kama unakiwango sahihi pH.
3.Onana na wataalamu karibu yako kwa ushauri juu ya matumizi sahihi ya mbolea na mbolea sahihi.


No comments:

Post a Comment