Monday, 9 April 2018

FAIDA ZA TANGAWIZI.

Habari za siku ya leo ndugu msomaji.
leo tutaangalia umhimu wa tangawizi katka afya yako.
Faida za tangawizi ni pamoja na:
1.      Inasaidia kuondoa kichefuchefu.
Kwa utafiti uliofanyika uingereza kwa kuwashirikisha wajawazito 1278 na kugundua kuwa tangawizi ilikuwa na uwezo wa kuondoa kichefuchefu na pia utafiti kama huo ulifanyika katika chuo kikuu ch afya cha Rochester ulionyesha kuwa tangawizi iliweza kuondoa kichefuchefu kwa wagonjwa waliokuwa wakipata matibabu ya mbalimbali. (1) (2)
2. Huweza kupambana na maambukizi ya fangasi.
Tangawizi ina kemikali inayoweza kupambana na fangasi wa aina mbalimbali.mfano utafiti uliofanyika nchini Iran mwaka 2016 ulionyesha kuwa tangawizi ilikuwa na uwezo wa kupambana na aina kadha ya fangasi wanaosababisha magojwa ya midomo. (3),pia utafiti kwenye mimea zaidi ya 29 uliweza kuonyesha kuwa tangawizi ilikuwa na uwezo wa kuua kabisa fangasi. (4)
3. Huweza kuzuia vidonda vya tumbo
Tangawizi huweza kuzuia kutokea kwa vidonda vya tumbo kwa kisi kikubwa kwa mfano ni ule utafiti uliofanyika mwaka 2011 ulinesha kwa tangawizi ina uwezo mkubwa wa kuzuia chemicali za tumbo zinazoweza kusababisha vidonda vya tumbo. (5)
4. Huweza kupunguza maumivu ya wakati wa hedhi.
Wanawake wengi huweza kupata maumivu wakati wa hedhi yakiambatana na maumivu ya kichwa,wengi hutumia dawa za madukani,lakini habari njema ni kuwa tangawizi huweza kupunguza maumivu hayo na kufanya kipindi cha hedhi yako kuwa murua.
Uchunguzi uliochapishwa kwenye jarida la “Alternative and Complementary Medicine” (6  lilionyesha kuwa tangawizi ina uwezo wa kuondoa maumivu ya wakati wa hedhi.
5. Huweza kuzuia kukua na kuopngezeka kwa seli za kansa.
Uwepo wa chemikali ya 6-gingerol ambayo ni humhimu kwa ajili ya kupambana na kansa.

6. Huweza kurekebisha kiwangao cha sukari mwilini.

Kwa wale wenye kisukari tangawizi ni mhimu sana kwa kurekebisha kiwango cha sukari katika mwili na kuweza kuzuia athari zaidi zinazo weza kutokea kama uharibifu wa mfumo wa fahamu unaoweza kuleta kiharusi na kuweza kuchelewa kupona kwa vidonda

7. Huweza kupunguza maumivu ya misuli.

Kwa sababu ya uwezo wake wa kupunguza uvimbe ,tangawizi kwa kuchanganya kwenye chakula huweza kupunguza maumivu ya mishipa na misuli.

8. Hupunguza kiwango cha mafuta mabaya (cholesterol) mwilini.
Mafuta mabaya mwilini huweza kusababisha matatizo ya moyo na shinikizo la damu,kwa kuweza kutumia tangawizi, ni rahisi kupunguza lehemu na kuepukana na athali zinazoweza kuambatana na magonjwa hayo.

9. Ina uwezo wa kurekebisha mfumo wa ubongo.

Utafiti uliofanyika mwaka 2012 uliweza kuonyesha kuwa watumiaji wa tangawizi huwa na uwezekano mdogo wa magonjwa ya akili,kuzeeka kwa ubongo nk.

Faida zngine ni pamoja  na kupambana na magonjwa ya bacteria,kuweza kupunguza uvimbe pia husaidia kuwezesha umeng’enyaji mzuri wa chakula..

No comments:

Post a Comment