WADUDU
WASUMBUFU WA VIAZI MVIRINGO
1. Wadudu nondo (Potato tuber month)
Wadudu nondo kitaalam kama (Phthoremaea
operculella) hupatikana katika maeneo ya kuhifadhia viazi hasa kwenye
maghala na katika mashamba ya viazi. Wadudu hawa athari zake hazionekani kwa
urahisi, pia kiazi kilichoshambulia na wadudu hawa, huweza kuota shambani,
lakini viazi vilivyoathrika huanza kuoza mara tu vinapovunwa na kuwekwa kwenye
ghala. Wadudu hawa ni hatari sana hasa kwa wakulima wa mbegu za viazi, kwani
hupunguza ubora wa mbegu, hali inayopelekea kushuka hata kwa bei ya mbegu hizo,
na wakati mwingine kukataliwa na wakaguzi wa mbegu.
DALILI
ZA UHARIBIFU
Wadudu nondo huathiri viazi na majani.
Mabuu hushambulia sana viazi vikiwa shambani au vikiwa kwenye ghala. Hata
hivyo, dalili nyingi za wadudu hawa hutokea kwenye ghala.Kinyesi cha wadudu
hawa huweza kuonekana juu ya kiazi cheyewe.
Wadudu hawa pia hushambulia mashina na majani ya viazi.
Jinsi
ya kudhibiti wadudu nondo
1. Kwa
kutumia mbegu iliyo safi na isiyokuwa na maginjwa.
2. Kuteketeza
viazi na mimea yote ya viazi iliyoathrika
3. Kuweka
matuta mara tu baada ya kupanda. Hii huzuia wadudu nondo kutaga mayai juu ya
viazi, kisha kuzalisha viwavi ambao wataingia ndani ya kiazi na kuzaliana.
4. Kukata
mashina ya viazi siku 90 baada ya kupanda. Hii huzuia mabuu kwenye majani kutoka
kuhamia kwenye viazi na kwenye udongo
5. Kutumia
kilimo cha mzunguko wa mazao - Mzunguko wa mimea ni njia nzuri ya kuvunja
mzunguko wa uzazi wa wadudu nondo.
Wadudu
mafuta (aphid)
Wadudu hawa mara zote hawawezi
kukosekana ndani ya shamba la viazi mviringo, wadudu mafuta huanza kushambulia
mimea ya viazi tangu kuchipua hadi kukomaa kwa viazi. Mwonekano wao ni wadogo
sana, laini na wenye rangi ya kijani-njano. Wakishakuwa wakubwa wadudu hawa
huweza kuruka kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine, wakiambukiza na
kusambaza magonjwa.
DALILI
ZA UHARIBIFU
Mara nyingi wadudu mafuta wanapokuwa
kwenye mimea, huwa wanafyonza maji maji yote kwenye mashina na majani tete,
hali ambayo husababisha kukauka kwa majni yaliyokwisha kutokeza. Pia huzuia
kufunguka kwa majani yanayotokeza kwenye incha.
Wadudu mafuta wenye mabawa huweza kuruka
na kueneza magonjwa ya virusi, kwenye mmea mwingine, endapo atakuwa amefyonza
virusi kutoka kwenye mmea uliokwisha ambukizwa na magonjwa ya virusi.
Jinsi
ya kudhibiti wadudu mafuta
Wadudu mafuta wanaweza kudhibitiwa kwa
kupuliziwa madawa ya kuulia wadudu kama Selecron, au Dimethiote. Pia wadudu
hawa huwa wanaondolewa shambani kama shamba litakuwa na wadudu wanaoitwa mende
wa viazi (Potato corrolado bettle). Mende hao chakula chao kikuu ni wadudu
mafuta, hivyo mkulima anaweza kutambua kuwa shamba lake halina wadudu mafuta
iwapo shambani kutakuwa na hawa mende wa viazi. Pia mkulima iwapo hatawadibiti
hawa mende wa viazi, wakimaliza kula wadudu mafuta, mwishowe huanza kutoboa
majani ya viazi, kisha na kusababisha kukauka kwa kwa mmea.
Wadudu
chiriku (Thrips)
Wadudu hawa ni wadogo sana kwa umbo,
wenye tumbo refu na huwa wenye rangi ya manjano na wangine wana rangi nyeusi.
Wadudu hawa mar azote hupatikana kwenye
mimea ya viazi tangu ikiwa kama machipukizi mpaka kukomaa kwa viazi.
DALILI
ZA UHARIBIFU
Kama ilivyo kwa wadudu mafuta, wadudu
chiriku pia kusababisha uharibifu kwa mimea ya viazi.
Wadudu hawa huaribu sehemu ya chini ya
majani, kisha hufyonza majimaji yote haliyopo kwenye majani mapya na yaliyo
laini, hali ambayo husababisha kukauka kwa mimea.
Vile vile wadudu chiriku wanaweza kubeba
na kuenea magonjwa ya virusi kwenye shamba la viazi.
Jinsi
ya kudhibiti wadudu chiriku
Wadudu hawa wanaweza kudhibitiwa kwa
kufanya haya yafuatayo:
• Kwa kupulizia madawa ya kuulia wadudu
• Kilimo cha mzunguko wa mazao
Viwavi
au (cutworm)
Wadudu hawa mara nyingi hupatikana ndani
ya udongo, na kuwepo kwa wadudu hao, wanaweza kuanza kukata mashina ya mimea
tangu inapochipua mpaka kuvuna. Viwavi kuharibu si tu mimea ya viazi mviringo,
pia kuathiri karibu kila aina ya mimea ikiwa ni pamoja magugu.
DALILI
ZA UHARIBIFU
Wadudu hawa huharibu mashina ya mimea na
mizizi. Dalili huoneka na kwenye mimea baada ya kuona baadhi ya mashina
yamekatwa mara tu bada ya kuchipua. Wadudu hawa wanaweza kusababisha hasara
kubwa shambani; hasa wakati mimeaina siku 25-35 tangu kupandwa kwa viazi.
Jinsi
ya kudhibiti wadudu viwavi
Ili mkulima kuweza kudhibiti wadudu
hawa, yafaa kufanya haya yafuatayo;-
1.
Kuondoa na kutaketeza mabuu yote yanaoonekana
shambani hasa wakati wa kuandaa shamba na wakati wa kuwekea matuta.
2.
Kupulizia madawa ya kuulia wadudu
shambani kabla ya kupanda.
Inzi
weupe (whitefly)
Nzi weupe huathiri si tu viazi mviringo
bali hata na mazao mengine ya mboga na nafaka.
DALILI
ZA UHARIBIFU
Nzi weupe huathiri mimea ya viazi kwa
kufyonza majimaji kwenye majani machanga. Majani yaliyoathirika huwa dhaifu na
hatimaye kukauka.
Jinsi
ya kudhibiti inzi weupe
Inzi weupe huweza kudhibitiwa kwa
kupulizia dawa ya kuulia wadudu kama ilivyokwisha tajwa hapo mwanzo.
Matumizi
ya viuatilifu vya wadudu
Utangulizi:
Kiuatilifu kwa kawaida siyo dawa bali ni
sumu ambayo inaweza kuua aina yoyote ya viumbe hai. Viuatilifu ni kwa ajili ya
kuulia wadudu, na vinatumika sana pasipo kufuata maelekezo. Kwa wakulima wa viazi hasa kipindi cha mvua
wanaweza kupulizia dawa hata mara mbili kwa siku. Pia wakulima walio wengi
huchanganya aina mbalimbali za viuatilifu wakati wa kutumia shambani.
Kwa ujumla mkulima akichanganya aina
mbali mbali za viuatilifu, hupunguza ufanisi wa kiuatilifu, n ahata hivyo kwa
kufanya hivyo, huongeza gharama za uzalishaji wa viazi.
AINA
ZA VIUATILIFU
Viuatilifu vya kemikali vinaweza kuwekwa
katika makundi mbali mbali kutokana na lengo la matumizi kwa mkulima.
• Kiuatilifu cha kuua wadudu
(Insectcides).
• Kiuatilifu kwa ajili ya kuua magugu
(Herbicides)
• Kiuatilifu chaye lengo la kutokomeza
fangasi (Fungicides).
• Kiuatilifu cheye lengo la kutokomeza
minyoo fundo (Nematicides)
VIUATILIFU
KULINGANA NA UTENDAJI KAZI WAKE
• Kiuatilifu kinachongandia (Contact
pesticides)
Kiuatilifu hiki hufanya kazi kwa
kugusana na sehemu yenye ugonjwa. Dawa hizi hubaki kwenye mimea tu baada ya
kupulizwa, lakini ni bora na huyafa kazi kwa muda mfupi.
• Kiuatilifu cheye kupenyeza (systemic
pesticide)
Hii ni dawa ambayo inaweza kuingia na
kupenyeza ndani yam mea na kusambaa sehemu zote za mmea wa kiazi. Kiuatilifu
hiki ni kizuri kwani kinatibu na kukinga wadudu pamoja na magonjwa husika. Sumu
ya dawa hii hukaa kwa muda mrefu ndani ya mmea. Kiuatilifu hiki hakiruhusiwi
kutumika kwenye viazi vilivyo karibu kuvunwa, kwani sumu hukaaa kwa muda mrefu,
hivyo kusababisha athari kwa watakaotumia.
JINSI
YA KUTUMIA VIUATILIFU MBALIMBALI
Ili kuwa na ufanisi wa dawa za kuzuia na
kuua wadudu, hutegemea sana na jinsi mkulima anavyoitumia. Lini na wakati gani
dawa itumike ni vitu vya kuzingatia. Ili
kiuatilifu kiweze kufanya kazi vema, yafuatayo lazima yazingatiwe;-
1.
Kiuatilifu kilengwa: Kwa mfano, ili
kudhibiti wadudu mafuta, lazima dawa ya kuiua wadudu hao itumike. Kwa kawaida orodha ya viumbe hai husika
huonekana juu ya maandiko ya kifungashio.
2.
Majira sahihi: Majira lazima ni kitu cha
msingi kutokana na tabia ya wadudu walengwa na hali ya hewa wakati wa kupiga
dawa. Kama wadudu wanaonekana wakati wa asubuhi, ni bora kupiga dawa wakati wa
asubuhi pia. Hali ya hewa, hasa mvua na jua, vinaweza kuwa na ushawishi mkubwa
sana kwenye utendaji wa kazi ya kiuatilifu.
3.
Kiasi sahihi: kwa kawaida kila
kiuatilifu huwa kinamaelezo ya kiasi cha kutumia. Maelezo hayo huwekwa juu ya
kifungashio. Hayo maelezo ni lazima kuzingatiwa na mkulim. Mkulima asipo fuata
maelekezo ya dawa, basi husababisha dawa isiweze kufanya kazi vizuri, na
hutengeneza sugu au ukizani dhini ya ugonjwa au wadudu husika.
4.
Kuchangaya: Viuatilifu havipaswi
kuchanganywa wakati wa kutumia, kwani huchangia kupunguza uwezo wa dawa katika
kufanya kazi. Na kutengeneza sumu mbaya, inayoweza kuua hata na viumbe
visivyolegwa.
Hatari
za viuatilifu kwa binadamu na mazingira
Hatari ya madawa ya kuulia wadudu kwa
binadamu na mazingira ni:
• Sumu kwa binadamu: Wakulima hutumia
madawa ya kuulia wadudu na magonjwa bila ya kuwa na kinga. Husababisha kifo,
lakini inaweza kusababisha pia magonjwa ya ngozi kama kansa, kichefuchefu,
udhaifu mwilini, maumivu ya kichwa, degedege.
• Kuua viumbe wengine.
• Maji na uchafuzi wa hewa.
No comments:
Post a Comment