UTANGULIZI
Tanzania ina idadi ya
kuku wa kienyeji wanaokadiriwa kuwa million 34 ambao wanafugwa kwa mtindo wa
huria. Ufugaji wa aina hii hufanyika vijijini na mijini pia.
Idadi hii ya kuku bado
ni ndogo ikilinganishwa na mahitaji halisi ya Watanzania wanaokadiriwa kuwa
milioni 45 Ulaji wa nyama ya kuku nchini unakadiriwa kuwa ni wastani wa kilo
0.7 kwa kila mtu kwa mwaka mzima ilihali Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja
wa Mataifa (FAO) linakadiria wastani mzuri wa ulaji wa nyama kuwa ni kilo 6.8
kwa mtu kwa mwaka. Hii inaashiria kuwa soko la kuku nchini ni kubwa, ambayo ni
fursa muhimu kwa wafugaji wa kuku.
Ufugaji wa kuku ni
nyenzo nzuri ya kujipatia kipato katika kaya kwa sababu ufugaji wa kuku
hauhitaji mtaji mkubwa na hauna kazi kubwa kiuendeshaji. Katika ufugaji huria,kuku
hujitafutia chakula wenyewe. Pia inapowezekana hupewa mabaki ya chakula,
chenga, pumba au nafaka yoyote inayopatikana katika mazingira husika. Kwa walio
wengi ifikapo nyakati za jioni, kuku hulala jikoni au ndani nyumbani kwa mfugaji
mwenyewe. Ufugaji huu ni rahisi kwa kuwa hauna gharama kubwa ila faida yake ni
kitoweo tu au fedha kidogo sana.
Kutokana na lishe duni
na kuzaana wenyewe kwa wenyewe (bila kubadili jogoo), kuku wa kienyeji walio
wengi wana uzito mdogo. Wana wastani wa uzito wa robo tatu za kilo hadi kilo
moja wakiwa na umri wa zaidi ya mwaka mmoja. Ila wakitunzwa vizuri zaidi na
kuboreshwa wana uwezo wa kufikia uzito wa kilo moja hadi moja na nusu katika
umri wa miezi sita hadi nane.
Kwa upande wa utagaji
wa mayai kuku wa kienyeji kwa wastani hutaga mayai 50 hadi 65 kwa mwaka.
Wakitunzwa vizuri zaidi huweza kufikia uzalishaji wa mayai 80 hadi 100 kwa mwaka.
Kijitabu hiki kinatoa
maelezo ya njia na kanuni mbalimbali rahisi za kuzingatia ili mfugaji aweze kuzitumia
kupata mazao mengi na bora zaidi yatakayomnufaisha kimapato na kwa matumizi
mengine.
Kanuni hizi ni pamoja na:
v Kuchagua njia bora ya kufuga na sifa za
mabanda bora ya kuku
v Kuchagua aina bora ya kuku wa kufuga,
kuzaliana na kutotolesha
v Utunzaji wa vifaranga.
v Kutengeneza chakula bora cha kuku
v Kudhibiti na kutibu magonjwa
v Kutunza kumbukumbu
v Kutafuta masoko
NJIA TOFAUTI ZA
KUFUGA KUKU.
Mambo yanayomfanya
mfugaji kuamua atumie njia fulani ya kufuga ni pamoja na uwezo wa kugharamia shughuli ya ufugaji wa kuku na
ukubwa wa eneo alilonalo la kufugia. Katika sehemu hii utajifunza njia tatu za
kufuga kuku ambazo ni:
1.
Kufuga huria.
Kuku huachwa wenyewe
kujitafutia chakula na maji. Njia hii inatumika zaidi kufuga kuku wa kienyeji.
Mara chache sana mfugaji huwapatia kuku chakula cha ziada. Kwa ufugaji huu
lazima kuwe na eneo kubwa la kutosha kuku kuzunguka na kutafuta chakula. Kuku hulala
eneo lisilo rasmi
kama vile jikoni, kwenye kiambata n.k.
Faida zake
• Ni njia rahisi ya kufuga.
• Gharama yake pia ni ndogo.
• Kuku wanapata mazoezi ya kutosha.
• Kuku wanapata chakula mchanganyiko ambacho
kinafaa kiafya.
Hasara zake
• Kuku huwa hatarini kuibiwa au kudhurika na
wanyama wakali na hali mbaya ya hewa.
• Ukuaji wa kuku ni hafifu, hufikia uzito wa
kilo 1.2, baada ya mwaka.
• Huharibu mazingira kama kula na mimea ya bustanini
mazao kama nafaka.
• Ni rahisi kuambukizwa magonjwa.
2.
Kufuga nusu ndani – nusu nje
Huu ni mtindo wa kufuga ambapo kuku wanakuwa na
banda lililounganishwana uzio kwa upande wa mbele. Hapa kuku wanaweza kushinda
ndani
Wakati wa mchana kuku
huwa huru kushinda ndani ya banda hasa wanapotaka kutaga na wakati wa kuatamia
au wanaweza kukaa ndani ya uzio nje.
Faida za kufuga nusu
ndani na nusu nje
• Kuku wanakuwa salama mbali na maadui mbali
mbali.
• Utaweza kuwalisha kuku wako vizuri hivyo
wataweza kuongeza uzalishaji wa mayai na wa nyama (kwa kukua haraka).
• Itakuwa rahisi kwako kudhibiti wadudu na
vimelea vinavyoweza kuleta magonjwa kwa kuku wako.
• Ni rahisi kuwatenganisha kuku katika makundi
tofauti na kuwahudumia ipasavyo.
• Ni rahisi kutambua kuku wagonjwa kuliko kufuga
huria.
• Kuku watapata mwanga wa jua wa kutosha pamoja
na hewa safi.Wakati wa jua kali watakuwa huru kuingia ndani ya banda na kukaa
kivulini.
• Kuku hawatafanya huharibifu wa mazao yako
shambani au bustanini na kwa majirani zako.
• Utapata urahisi wa kukusanya na kupeleka
mbolea bustanini au shambani.
Changamoto ya kufuga
nusu ndani na nusu nje
• Huna budi uwe na muda wa kutosha kwa ajili ya
kuwahudumia kuku wako.
• Pia utahitaji kuwa na eneo kubwa kiasi la
kufugia.
• Pia utaingia gharama ya ziada kidogo ya
kutengeneza banda na wigo na kuwapatia uku chakula cha ziada.
• Hata hivyo gharama za muda huo na za vifaa
vingine zita?diwa na mapato ya ziada utakayopata kwa kufuga kwa njia hii.
3.
Kufuga ndani ya Banda tu
Njia nyingine ni
kuwafuga kuku ndani tu. Katika njia hii, kuku hukaa ndani wakati wote. Njia hii
ya ufugaji utumiwa zaidi na wafugaji wa kuku wa kisasa. Lakini yaweza kutumika
hata kwa kuku wa asili hasa katika sehemu zenye ufinyu wa maeneo.
Changamoto za ufugaji
wa ndani ya banda tu
• Unatakiwa uwe na muda wa kutosha wa
kuwahudumia kuku wako kikamilifu.
• Pia unatakiwa kuwa na mtaji mkubwa wa kujenga
banda na kuwanunulia kuku chakula.
• Ugonjwa ukiingia na rahisi
kuambukizana.Vilevile kuku huweza kuanza tabia mbaya kama kudonoana, n.k.
Faida za kufuga ndani
tu
• Ni rahisi kutambua na kudhibiti magonjwa.
• Ni rahisi kudhibiti upotevu wa kuku, mayai na
vifaranga.
• Ni rahisi kuwapatia chakula kulingana na
mahitaji ya kila kundi.
• Ni rahisi kuwatambua na kuwaondoa kuku
wasiozalisha katika kundi.
Ni ufugaji upi unafaa zaidi kutumika kwenye mazingira ya vijijini?
Kwa ujumla, njia rahisi
na inayopendekezwa kutumiwa na mfugaji wa kawaida kijijini ni ya ufugaji wa
nusu ndani na nusu nje, yaani nusu huria. Hii inatokana na faida zake kama
zilizoainishwa hapo awali. Kwa kutumia mfumo huu wa ufugaji, utaepuka hasara za
kufuga kwa mtindo wa huria kama zilivyainishwa mwanzoni mwa sehemu hii ya
kitabu hiki.
Pia ukitumia mtindo wa
ufugaji wa nusu huria utafanya ufugaji wako kwa njia bora zaidi ndani ya uwezo
ulionao, kwa sababu kwa sehemu kubwa utatumia mali ghafi inayopatikana katika
eneo lako.
KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU
Watu wengi hapa nchini hujihusisha na ufugaji wa kuku kwa lengo la
kujipatia chakula na kipato. Mazao yatokanayo na ufugaji wa kuku ni pamoja na
mayai, nyama, mbolea na manyoya kwa matumizi mbalimbali. Mifumo ya ufugaji kuku
ambayo hutumika hapa nchini ni huria, nusu huria na shadidi. Ufugaji wa kuku
utakuwa endelevu na wenye tija kwa kufuata kanuni za ufugaji bora zifuatazo:-





1 Banda la Kuku
Kuku huhitaji banda bora ili wasiathirike na madhara mbalimbali.
Banda bora la kuku linatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:-
ü Imara, lenye uwezo wa kuwahifadhi kiafya na pia dhidi ya hali ya
hewa hatarishi kwa mfano jua kali, upepo, baridi na mvua pamoja na wanyama
hatari,
ü Lenye mwanga, hewa na nafasi ya kutosha inayoruhusu usafi kufanyika kwa urahisi,
ü Lijengwe sehemu yenye mwinuko isiyotuama maji, isiyo na upepo
mkali na iwe mbali kidogo na nyumba ya kuishi watu,
ü Liwe na vichanja kwa ajili ya kuku kupumzika na kulala
ü Liwe na sehemu ya kuwekea chakula, maji, kutagia, kuatamia na
sehemu ya kulelea vifaranga,
ü Liwe na nafasi ya kutosha
kulingana na idadi ya kuku na kuweka
vyombo vya chakula na maji,
ü Kwenye mazingira ya joto banda liwe la ukuta mfupi na sehemu ya kubwa
wazi yenye wavu hadi kufikia kwenye paa
ü Kwenye mazingira ya baridi banda liwe na ukuta mrefu unaokaribia
paa na sehemu ndogo tu iwe wazi yenye wavu ili kupitishia hewa na mwanga.
1.1 Vifaa Vinavyotumika
kwa Ujenzi wa Banda
Vifaa vya kujengea
banda vizingatie gharama na upatikanaji wake katika eneo husika. Baadhi ya
vifaa hivyo ni kama ifuatavyo:-
v Sakafu -
Saruji, udongo, mbao, mianzi au fito
v Kuta - Fito, mabanzi, mbao, nguzo mianzi, udongo,
matofali, mawe, mabati na wavu
v Paa -
Nyasi, makuti, majani ya migomba, mabati na vigae.
v Wigo - Matofali, mbao, fito
nguzo, mabanzi, mianzi,matete, wavu na
mabati
Vyombo vya Maji
kuku ya kunywa.
• Aina ya mojawapo unayoweza kutumia ndoo au debe la lita kumi au ishirini
ya plastiki. Kata ndoo hiyo pande nne
kutoa nafasi ya kuku ya kunywea kama kielelezo
kinavyoonyesha. Tengeneza idadi ya vyombo hivi inayowiana na wingi
wa kuku ulionao.
• Au waweza kutumia sufuria au beseni pana
kiasi. Hii huwekewa tofali au jiwe sa? pana baada ya kuwekewa maji ya kunywa
ili kuzuia kuku wadogo wasizame na maji yasichafi liwe kirahisi.
• Vifaa maalum vya kunyweshea kuku vinapatikana
katika maduka ya pembejeo za kilimo.
Vyombo vya Chakula
ili kupata chakula cha chini.
Tabia hii husababisha kumwagwa kwa
chakula kingi chini na kusababisha hasara. Unaweza kudhibiti tatizo hili kwa
kutengeneza vyombo visivyoruhusu kuku kuchakura kama inavyoonyeshwa kwenye
kielelezo hapa chini.
Unaweza kutengeneza kilishio hiki
wewe mwenyewe au fundi seremala waliopo katika eneo unaloishi. Inafaa kilishio kiwe
chembamba ili kuku wasiweze kuingia. Pia kinatakiwa kiwe kirefu ili kuku waweze
kula bila kusongamana.
Viota
Zipo aina tofauti za viota ambazo
hutumika kwa ajili ya kutagia. Ipo aina ya ambayo ni ya kutagia kuku mmoja mmoja. Vipimo
vinavyopendekezwa kwa kila kiota ni upana wa sentimita 30, urefu sentimita 30
na kina sentimita 35. Upande wa mbele uachwe wazi
ila
sentimita 10 za kwanza kutoka chini zizibwe na ubao Weka idadi ya viota
inayotoshelezakuku ulio nao.
Pia ipo aina nyingine inayoweza kutumiwa na kuku zaidi ya mmoja
kwa wakati mmoja. Ni kama kiota kimoja kilichogawanywa katika vyumba kadhaa.
Ila kila chumba kina vipimo kama vya kiota kimoja (angalia picha hapa
chini).Aina hii ya kiota ina upanawa sentimita 30 na kina sentimeta 35na urefuwake
unategemea idadim ya viota.
Vichanja
Kuku wana asili ya kupenda kulala au
kupumzika sehemu iliyoinuka. Hivyo ndani ya banda weka vichanja
vitakavyotosheleza idadi ya kuku waliopo.
UCHAGUZI WA KUKU BORA.
Kuku wa Asili
Aina za kuku wa asili wanaopatikana hapa nchini ni pamaja na Kuchi
(Kuza), pori (Kishingo), Njachama,
Kinyavu, Mbuni na Tongwe (Msumbiji). Mfugaji anaweza kuongeza uzalishaji kwa
kuchagua kuku mwenye sifa zifuatazo:-
ü Uwezo wa kutaga mayai mengi
(kati ya 15-200 katika mzunguko mmoja wa utagaji
ü Uwezo wa kuatamia na kuangua vifaranga wengi,
ü Uwezo wa kustahimili
magonjwa
ü Umbo kubwa na kukua haraka.
Masuala ya
Kuzingatia Wakati wa Kumchagua Kuku Mtagaji Asili.
Viungo vya
mwili Sifa:
v Macho Maangavu, yenye wekundu kwa mbali na makubwa yamejaa kwenye
soketi za macho.
v Mdomo Wenye rangi ya njano kwa mbali
v Kisunzu/Upanga Chekundu,
Laini,kimelala kidogo upande na kinang’aa Shingo Iliyosimama ,
v Umbali kati ya kidali na nyonga , Upanga wa vidole 3-4 vya
mpimaji,
v Upanga wa nyonga Upana wa vidole 3 vya mpimaji.
Kuku wa Kisasa
Kuku bora wa kisasa kwa ajili ya mayai au nyama ni mwenye sifa
zifuatazo:-
Ø Uwezo wa kuanza kutaga wakiwa na umri mdogo (miezi 5-6) kutegemea na
koo,
Ø Umbo kubwa na anayekula
haraka (kilo 1.5-2.0 kwa kipindi cha wiki 8-120 kutegemea na koo kwa kuku wa
nyama,
Ø Anayetaga mayai mengi (250 au zaidi) kwa kuku wa mayai kwa mwaka;
na
Ø Awe na uwezo wa kutaga katika umri wa miezi 6-8.
Uchaguzi wa Jogoo Bora wa Mbegu
Jogoo wa mbegu anatakiwa awe na sifa zifuatazo:-
Ø Achaguliwe kutoka kwenye koo zenye sifa ya kutaga mayai mengi,
Ø Mrefu, umbo kubwa, miguu imara na yenye nguvu,
Ø Awe machachari, ushawishi kwa mitetea na ari ya kupanda
Ø Uwezo wa kupanda akiwa na umri wa miezi 7-10.
Uchaguzi wa Mayai kwa ajili ya Kutotoa Vifaranga.
Mayai kwa ajili ya kutotoa vifaranga yawe na
sifa zifuatazo:-
Ø Yaliyorutubishwa na jogoo,
Ø Yasiwe na nyufa,
Ø Yasiwe na maganda tepetepe,
Ø Yasiwe na kiini kilichovunjika,
Ø Yawe na ukubwa wa wastani; na
Ø Yasiwe yamekaa zaidi ya wiki 2 baada ya kutagwa.
Utunzaji wa Mayai
Mayai ya kienyeji kwa ajili ya kutotoa vifaranga yatunzwe kwa
kusimamishwa wima sehemu iliyochongoka ikiwa imeangalia chini kwa siku 3 za
mwanzo na kisha yageuzwe ili sehemu iliyobutu iangalie chini. Mayai yahifadhiwe
kwenye sehemu iliyo na ubaridi kidogo na giza.
Utunzaji wa Kuku kwa
Makundi
Utunzaji wa Vifaranga.
Malezi bora ya vifaranga ni muhimu katika ufugaji wa kuku kwa
sababu vifaranga hawana uwezo wa
kustahimili mazingira wakiwa wenyewe mara wanapoanguliwa.Ukosefu wa malezi
bora husababisha vifaranga kuwa
dhaifu,kufa kwa wingi na hivyo kupunguza idadi ya kuku wa baadaye. Malezi ya
vifaranga yanaweza kufanyika kwa kutumia kuku walezi au kutumia vifaa maalum.
Kulea Vifaranga kwa
Kutumia Kuku Mlezi
Vifaranga wanaweza kulelewa na mama yao au kuku mlezi. Endapo kuku
wengi wametotoa vifaranga kwa wakati mmoja, achaguliwe kuku mlezi aliye na
uwezo wa kulea vifaranga wengi kati ya
waliototoa aendelee kulea na wengine waliototoa waachwe huru ili warudi kwenye
mzunguko wa kutaga. Kuku mmoja anaweza kulea vifaranga 20 hadi 25. Mfugaji wa
kuku,pamoja na kanuni nyingine, anapaswa kuzingatia yafuatayo:-
Ø Kuku anayelea vifaranga atengewe chumba maalumu, apewe maji ya
kutosha na chakula chenye virutubisho muhimu,
Ø Vifaranga wasiachiwe kutoka nje hadi watakapofika umri wa wiki 6,
Ø Vifaranga watengwe na mama/mlezi baada ya wiki 4 kuruhusu mama
aendelee na mzunguko wa kutaga;na
Ø Katika maeneo yenye hali ya hewa ya ubaridi vifaranga wacheleweshwe
kutenganishwa na mama/mlezi hadi wiki ya 6 au mpaka waonekane
wameota manyoya ya
kutosha.
Bruda ni chombo/sehemu iliyoandaliwa mahusus kwa ajili ya
kuwapatia joto vifaranga badala ya mama/mlezi. Mfugaji anaweza kulea vifaranga
wengi kwa kutumia bruda ambayo ni mduara unaweza kutengenezwa kwa kutumia mbao,
karatasi ngumu au kwa kuziba pembe za chumba.Aidha, njia hii hupunguza vifo vya
vifaranga vinavyosababishwa na ndege au wanyama hatari,huruhusu kuku kutaga
mapema zaidi na kuwa na mizunguko mingi ya utagaji (kwa kuku wanaoatamia).
Vilevile, hurahisisha udhibiti wa magonjwa.
Mfugaji anapaswa kufuata
taratibu zifuatazo katika kulea vifaranga kwa kutumia bruda:-
v Kuweka vifaa vya kuongeza joto kwa mfano taa ya umeme, chemli au
jiko la mkaa. Zingatia kiwango cha joto kinachohitajika katika bruda.
v Wiki ya kwanza ni 35o c,
wiki ya pili ni 33o c, wiki ya tatu ni 31o c na wiki ya nne ni 29o c,
v Kuchunguza mtawanyiko wa vifaranga ndani ya bruda ili kutathimini
hali ya joto.Wakijikusanya kwenye chanzo cha joto, inaashiria kuwa baridi
imezidi hivyo joto liongezwe. Wakiwa mbali na chanzo cha joto maana yake joto
limezidi hivyo joto lipunguzwe,
v Bruda iwe na sakafu yenye malalo yatokanayo na maranda ya mbao au
pumba za mpunga. Malalo yabadilishwe endapo yataonekana yameloana,
v Bruda iwekwe vifaa vya maji na chakula. Maji na chakula kiwekwe
kabla ya kuweka vifaranga,
v Vifaa vya joto viwekwe ndani ya bruda masaa 6 kabla ya kuingiza
vifaranga,
v Vifaranga walishwe chakula cha kuanzia gramu 12-15 kwa kipindi cha
wiki ya 2. Katika wiki ya 3 wapewe gramu 21-35 kwa kifaranga na chakula hicho
kiwepo muda wote,
v Vifaranga wapatiwe vitamin, madini na dawa za kinga (antibiotics);
na
v Vifaranga wapatiwe chanjo kulingana na maelekezo ya mtaalamu wa
mifugo.Chanjo dhidi ya magonjwa muhimu kwa mfano,Marek’s (mara anapototolewa),
Mdondo (siku ya 3-4 na kurudiwa baada ya siku
ya 21 na kila baada ya miezi 3)
na Gumboro (siku ya 7na kurudia tena siku ya 21).Wapatiwa dawa ya minyoo (wiki
ya 8) na coccidiosis(wiki ya 3-4). Siku ya 45 wapewe chanjo ya ndui ya kuku.
Picha hapo juu kuonyesha mfano wa bruda
(kitalu).
Kutunza Kuku Wanaokua
(Wiki 8-18)
Utunzaji wa kundi hili unategemea mfumo unaotumika Kuku Wanaofugwa
Katika Mfumo Huria
Kuku wanaofugwa katika
mfumo huu wapatiwe matunzo bora yakiwemo yafuatayo;
v Wapewe chakula cha ziada asubuhi kabla ya kutoka na wanaporudi
kwenye banda. Chakula hicho kinaweza kugawanywa
mara ya 2 kwa siku,
v Wapatiwe maji safi na ya kutosha wakati wote
v Wapatiwe chanjo na dawa kulingana na ushauri wa mtaalam wa mifugo.
Wiki ya kumi warudie chanjo ya mdondo, wiki ya 12 kuhara (fowl cholera), wiki
ya 14 ndui ya kuku,
v Kuku Wanaofugwa Katika Mfumo Shadidi
v Majogoo watenganishwe na mitetea katika wiki 7 hadi 10 ili kuzuia uzaliano usio na
mpangilio,
v Wapewe chakula cha kukuzia kuanzia wiki ya 8-15 gramu 55- 60 na
kuanzia wiki ya 16 gramu 65-80 kwa wanaofugwa mfumo huria na gram 120-125 kwa
kuku kwa siku kwa wanaofugwa mfumo wa shadidi,
v Kuku wa nyama wapatiwe chakula cha kuku wa nyama muda wote,
v Wapatiwe maji safi ya kunywa
kwa muda wote kwenye vyombo safi,
v Kuku wachunguzwe dalili zozote za ugonjwa ili waweze kupata tiba
sahihi kutoka kwa mtalaamu wa mifugo,
v Kuku wa wiki 9-20 wanahitaji nafasi ya mita za mraba 0.15 kwa kuku
na wiki 21 au zaidi mita za mraba 0.25 kwa kuku,
v Kuwe na vyombo maalum vya kutosha kwa ajili ya chakula na maji,
v Wafanyiwe usafi wa banda mara kwa mara ili kuzuia magonjwa
yanayotokana na uchafu
v Wakatwe midomo ili kuzuia kudonoana.
Ukubwa wa Banda
Ukubwa wa banda utategemea idadi ya kuku na aina ya kundi la kuku.
Kuku wanahitaji nafasi tofauti kutegemea umri, aina na njia ya ufugaji. Eneo la
mita moja ya mraba linatosha kwa vifaranga 16 wa umri wa wiki 1 – 4. Hivyo
banda lenye mita za mradi 16
linaweza kulea vifaranga 320 hadi wiki 4. Baada ya wiki 4 eneo hili
liongezwe kutegemea aina ya kuku na njia
inayotumika katika ufugaji kama maelezo yanavyo onyesha hapo chini.
Eneo Linalohitajika
Kufuga Kuku Kwenye Sakafu ya Matandazo Kutegemea na Umri na Aina ya Kuku.
Umri wa Kuku Idadi ya Kuku
kwa mita 1 ya mraba Kuku wa mayai Kuku wa nyama
Siku1 hadi wiki 4
Wiki ya 5
hadi ya 8
|
9
|
Wiki ya 9
hadi 20
|
6
|
Wiki 21
kuendelea 3-4 -
|
-
|
Angalizo:
Mabanda yanayozungushiwa wigo kama ilivyo katika mfumo wa nusu
huria, kuku mmoja huhitaji eneo la wazi lenye ukubwa wa mita za mraba Mfano, kuku
100 huhitaji eneo la mita za mraba 1000
Utunzaji wa Kuku
Ulishaji
Kuku kama mifugo mingine uhitaji chakula chenye virutubisho vyote
vinavyohitajika mwilini ili kukua upesi na kuwa na na afya nzuri . Chakula kinachofaa ni mchanganyiko wa viini
lishe mbalimbali vyenye kazi tofauti mwilini. Kila kiini lishe hakina budi kiwe
katika kiwango sahihi kulingana mahitaji ya mwili wa kuku katika umri tofauti.
Kuku anahitaji chakula
chenye viini lishe vifuatavyo:
Kiini lishe
Wanga
Mafuta
Protini
Vitamini
Madini (calsium
na Fosforas)
|
Kinapatikana katika
chakula gani
Pumba,Chenga za nafaka kama
mahindi, mtama.
Mashudu yanayopatikana baada ya
kukamua mbegu za mafuta kama
alizeti, karanga n.k
Mashudu ya karanga au alizeti.Damu
iliyokaushwa ya wanyama kama
mbuzi, ng’ombe n.k. Mbegu za jamii
ya mikunde kama maharage, kunde,
soya....
Majani mabichi kama mabaki ya
mboga za majani, michicha ya porini,
majani mabichi ya mipapai, majani ya
Lusina n.k.
Unga wa dagaa, unga wa
mifupa
iliyochomwa, chokaa
|
Kazi yake mwilini
Kutia nguvu mwilini
Kutia nguvu na joto
mwilini
Kujenga mwili na
kukarabati mwili
Kulinda mwili. Majani
mabichi pia huwezesha
kuku kutaga mayai yenye
kiina cha njano, rangi
ambayo huwavutia walaji
wengi.
Kujenga mifupa,
kutengeneza maganda
ya mayai
|
Mfano wa kuandaa vyakula vya
makundi tofauti ya kuku
Kwa Vifaranga
Kwa
vifaranga vya tangu kutotolewa hadi miezi miwili, tengeneza mchanganyiko
ufuatao. Huu ni mfano mmojawapo wa kuandaa
kilo 100 za chakula cha vifaranga. Iwapo utahitaji kuandaa jumla ya kilo 50 za
chakula tumia nusu ya vipimo vilivyoainishwa katika jedwali hili. Wastani
wa mahitaji ya kuku wakubwa 50 kwa siku ni kilo 5. Chakula hiki ukigawe katika sehemu
mbili na kuwapatia nusu asubuhi na nusu ya pili mchana.
Vifaranga
hupewa chakula kiasi wanachoweza kumaliza (hawapimiwi).
Vifaa
Dagaa
(unga au vichwa vya dagaa)
Chenga
za nafaka kama mahindi au mtama n.k
Mashudu
Pumba
Chokaa
Unga
wa Mifupa,Madini ( Premix)
Chumvi
Mchanga
Jumla
|
Kiasi kwa kilo
12
hadi 15
40
20
24
2
2
Robo
kilo
1
Kilo 100
|
Kwa kuku wanaokua (baada ya miezi
miwili ).
Vifaa
Dagaa
(unga au vichwa vya dagaa)
Chenga
za nafaka kama mahindi au mtama n.k
Mashudu
Pumba
Chokaa
Unga
wa Mifupa,Madini ( Premix)
Chumvi
Mchanga
Jumla
|
Kiasi kwa kilo
7
30
20
39
2
2
Robo
kilo
1
Kilo 100
|
Kama umeamua kufuga kuku kwa mtindo
wa kuwaacha huru wajitafutie chakula (huria) unaweza kuwapatia vifaranga nyongeza
ya protini.Utafanya hivyo kwa kuwachanganyia vumbi au vichwa vya dagaa kiasi
cha kikombe kimoja vilivyotwangwa pamoja na pumba ya mahindi vikombe vitano.
Maji ya Kunywa
Mfugaji ahakikishe anawapatia kuku
maji masafi ya kunywa na ya kutosha kila siku. Vyombo vya maji ya kunywa budi visafishwe
vizuri kila siku. Hii itasaidia sana kudhibiti magonjwa yanayoweza kutokana na
vimelea vya magonjwa vinavyostawi katika maji yasiyo safi. Kuku wanaweza
kuwekewa maji katika aina tofauti ya vyombo kutegemea na urahisi wa kupatikana
mfano sufuria, ndoo za plastik zilizokatwa kuruhusu kuku kunywa bila kuchafua.
Usafi katika banda
Matandazo yanayowekwa katika sakafu
ya banda la kuku hayana budi yageuzwe mara kwa mara kwa wastani wa kila baada
ya miezi miwili au mitatu . Wakati mwingine ni kabla ya kipindi hiki muda
wowote yanapoloana na maji. Matandazo uharakisha kukauka kwa unyevu katika
banda unaotokana na kinyesi cha kuku na pia zaidi na maji yanayomwagika.
Usafi katika banda utasaidia
kudhibiti kwa kiasi kikubwa magonjwa mbalimbali. Kuokota mayai
Usiyaache mayai ndani ya viota kwa
muda mrefu, yaokote mara kwa mara ili kuepuka kuharibiwa kwa mayai hayo na kuku
wenyewe. Kuku wanayo tabia ya kula mayai yao ikiwa chakula unachowapa kina
upungufu wa protini.
Vilevile kiasi cha mwanga unaoingia
ndani ya banda kikizidi kuku hula mayai au kudonoana wenyewe kwa wenyewe.Uonapo
dalili za namna hii kwenye kundi lako punguza kiasi cha mwanga kwa kuziba
sehemu za madirisha kwa vipande vya magunia au vipande vya makasha ya karatasi
ngumu.
Kama ilivyoelezwa awali kuku wapewe
majani mabichi ya kutosha mara kwa mara ili wawe wanakula hayo badala ya
kudonoana.
Pia fuatilia kuhakikiksha kama
chakula kina protini ya kutosha. Kama tatizo la kudonoana na kula mayai litaendelea omba
msaada kwa mtaalam wa mifugo akuelekeze jinsi ya kuwakata au kuwachoma midomo.
Magonjwa ya Kuku
Magonjwa
ya kuku yapo mengi. Hata hivyo siyo yote yanatokea mara kwa mara hapa Tanzania.
IIi uweze kudhibiti yale yanayotokea katika kundi lako unahitaji kufahamu
dalili za jumla za magonjwa hayo. Unapoigundua moja au zaidi ya dalili za
ugonjwa au wadudu chukua hatua mara moja. Yapo magonjwa ambayo yanaweza
kuangamiza kundi lote la kuku katika.muda mfupi.
Jihadhari
na uwezekano wa kupatwa na hasara zinazoletwa na magonjwa ambayo unaweza
kuyazuia.
Katika
sehemu hii utajifunza kwa muhtasari tu dalili za jumla za magonjwa ya kuku na jinsi
ya kuyadhibiti.
Dalili za Jumla za Magonjwa ya
Kuku :-
• Kuku kupoteza hamu ya kula.
• Kuzubaa na kukaa mahali pamoja kwa muda mrefu
(Kutochangamka).
• Kushuka kwa kiwango cha utagaji wa mayai.
• Vifaranga kutokua upesi au kudumaa. - Macho
kuwa na rangi nyekundu.
• Kujikunja shingo.
• Kutetemeka, kutoa majimaji puani, mdomoni na
machoni.
• Kutoa mharo (kinyesi) wa rangi ya kijani au
wenye mchanganyiko na damu au cheupe.
• Kukonda.
• Kukohoa.
Ukion
Muhtasari wa Magonjwa Muhimu ya
Kuku na Jinsi ya Kuyadhibiti na Kutibu .
a
moja au zaidi ya dalili hizi katika kundi lako chukua hatua za kutibu
zilizoelezwa hapa chini. Kama hali ni ngumu
zaidi omba msaada kwa mtaalam wa tiba ya mifugo ili achunguze mara moja na
kukushauri jambo la kufanya.
Ugonjwa.
|
Chanzo.
|
Dalili.
|
Kudhibiti na Kutibu.
|
1.
Kideri
(Newcastle)
|
Virusi.
|
-Kukohoa,
kupumua kwa shida.
-Mwili
kukosa nguvu; -shingo kujikunja.
-Kuharisha
kijani.
-Kuku
hufa wengi
-Kuhara damu.
|
-Vifaranga
wachanjwe
katika
juma lao la
kwanza.
Chanjo la pili
wanapofikisha
umri wa
miezi
4 na nusu.
-Chanja kuku kila baada
ya miezi mitatu.
|
2. Kuhara damu
(Coccidiosis).
|
Bakteria.
|
-Kuku hujikusanya pamoja.
-Hawachangamki.
-Hushusha mbawa.
|
• Tunza usafi katika
banda.
• Lisha vifaranga chakula
kilichochanganywa
na dawa ya kinga
coccidiost kama
Amprolium au Salfa.
• Watenge kuku wote
Walioambukizwa na
wapatie dawa kama
Amprolium au salfa au
Esb3.
|
3. Ndui ya kuku
(Fowl pox).
|
Virusi.
|
-Malengelenge kwenye,kishungi na
kope za
macho na sehemu zisizo
na manyoya.
-Kuku uvimba uso na
Macho.
|
• Kuchanja kuku wote
wakiwa na umri wa
miezi miwili.
|
4. Mafua ya kuku
(Fowl coryza).
|
Bakteria.
|
-Kamasi hutirirka puani na
mdomoni
-Kuhema kwa shida hata
kukoroma.
-Kukohoa.
|
• Watibu wanaougua
kwa kutumia anti biotic
kama sulphamethazine,
streptomycine na
vitamin
• Usafi wa vyombo na
banda kwa ujumla
• Watenge kuku
wagonjwa
|
5. Kuharisha nyeupe
|
Bakteria.
|
-Kuharisha nyeupe na
hamu ya kula kupungua.
|
• Usafi wa vyombo na
banda kwa ujumla
• Watenge kuku
wagonjwa
• Tumia dawa kama
Furazolidone au
Sulfadimidine
• Hata vitunguu
|
Njia kuu za ujumla za kudhibiti
magonjwa ni:
Kutunza hali ya usa? ndani ya banda na kudhiditi
kusiwe na unyevu
Matandazo
yakichafuka yabadilishwe.
Vyombo vya maji visa?shwe kila siku
Jitahidi
uepuke kufuga kwa njia ya huria ili kuku wako wasiambukizwe magonjwa Kirahisi
Epuka
kufuga kuku wako pamoja na bata na khanga.Hawa ni wabebaji wa vimelea vya
magonjwa ya kuku japo wao hubaki
salama.
Zingatia
ratiba za chanjo kwa magonja yasiyo na tiba kama kideri na mengineyo ya virusi
Kutoa
chanjo ya kideri kwa njia ya kuweka matone ya dawa katika macho.
Ufugaji wa Aina Nyingine za Ndege.
Aina ya ndege wengine wanaofugwa hapa nchini ni pamoja na Bata
maji, Bata bukini, Bata bukini, Kanga na Njiwa. Ndege hao hufugwa kwa kiasi
kidogo ukilinganishwa na kuku kwa kuwa soko lao ni dogo.Utunzaji wao
hautofautiani sana na kuku;
v Wajengewe banda la kuishi ambalo ukubwa wake utagemea idadi ya
ndege wanaofugwa,
Mambo ya kuzingatia kwa
kuku wanaotaga ni pamoja na:-
v Banda liwe na viota vya
kutagia mayai (kiota 1 kwa kuku 3- 5).Viota viwekwe bandani mara kuku
watakapofikisha umri wa wiki 18 ili
waanze kuzoea kuvitumia,
v Wapatiwe chakula na maji
safi wakati wote kwa kutumia vyombo maalum ambavyo ni visafi,
v Kuku wasiotaga waondolewe kwenye kundi.Kuku hao
huonekana wasafi na sehemu ya kutolea yai huwa ndogo na kavu,upanga wake kichwa
(comb) huwa mdogo na mwekundu,
v Wapatiwe dawa ya minyoo
kila baada ya miezi 3,
v Wawekewe fito au ubao
mwembamba kama sehemu ya kupumzikia na mazoezi ili kuzuia kudonoana,
v Mayai yakusanywe mara 4 au
zaidi kwa siku ili yasidonolewe na kuku,
v Kuwe na malalo makavu na
yabadilishwe mara yanapochafuka,
v Vyombo vifanyiwe usafi kila
ili kuzuia magonjwa; na
v Watundikiwe majani mabichi
aina ya mchicha,papai, alfaafa,majani jamii ya mikunde ili kuboresha lishe.
Udhibiti na Tiba Dhidi ya Magonjwa ya
Kuku
Kuku wanaopata lishe bora, kutunzwa vizuri na kupatiwa chanjo
dhidi ya magonjwa yanayotokea mara kwa mara huwa na afya nzuri. Ni bora kuzuia
magonjwa kuliko kutibu ili kupunguza vifo na gharama. Iwapo ugonjwa utatokea
kuku wagonjwa watenganishwe na kuku wasio wagonjwa na wapatiwe tiba.
Kanuni muhimu za
kufuata ili kuzuia magonjwa ni:-
v Banda liwe safi muda wote,
v Kabla ya kuweka kuku, banda
linyunyuziwe dawa ya kuua wadau
wa magonjwa mbalimbali,
v Wapatiwe chakula chenye virutubisho na maji ya
kunywa yakutosha,
v Wapatiwe kinga na tiba dhidi ya magonjwa,
v Bata
maji na Bata
bukini wajengewe bwawa
lenye nafasi ya kukutosha kwa ajili ya kuogelea; na
v Njiwa
wajengewe viota sehemu
ya juu kama
kwenye mapaa ya nyumba.
Utunzaji wa Kumbukumbu.
Utunzaji wa kumbukumbu ni muhimu sana katika ufugaji wa kuku na
ndege wengine wafugwao
ili kusaidia mfugaji
kujua maendeleo ya ufugaji wake. Utaratibu wa kuweka
kumbukumbu mara tukio linapotokea ni lazima ili kuepuka kusahau.Mfugaji
ahakikishe anaweka kumbukumbu ambazo ni sahihi na zinazoeleweka.
Aina za Kumbukumbu
Kumbukumbu zinazopaswa
kuwekwa ni pamoja na:-






No comments:
Post a Comment