Wednesday, 1 March 2017

KILIMO BORA CHA MAHINDI

Mahindi ni lishe maarufu na muhimu kuliko zote Africa-jangwa la sahara, ni chakula kikuu kwa zaidi ya asilimia hamsini ya watu. Mahindi yana virutubisho vingi kama vile Wanga, Vitamini B, Protini, madini chuma na mengineyo ambayo ni muhimu katika kujenga mwili. Katika sehemu nyingi, mahindi huliwa katika mifumo tofauti; kwa mfano mahindi mabichi huchomwa, kuchemshwa au kukaangwa ili kuwa tayari kwaajili ya kuliwa, mahindi makavu husagwa na kutolewa unga au kukobolewa ambapo hutumika kama lishe. Kila sehemu ya mmea huu inatumika, kuanzia punje, majani, pumba, bua na gunzi zinaweza kutumika katika kutengeneza lishe ya binadamu, mifugo na matumizi mengine kama vile kuni.maeneo mbalimbali hapa duniani mahindi yanazalishwa zaidi MEXICO, U.S.A, BRAZIL,  ARGENTINA,INDONESIA NA EGYPT. Kwa TANZANIA mikoa inayozalisha zao hili la mahindi niRUVUMA, MBEYA, IRINGA, RUKWA na KIGOMA ambayo ndiyo mikoa inayochangia asilimia 40 ya uzalishaji wa zao hili la mahindi.
Hali ya hewa na mvua zinazohitajika ni kama zifuatazo
·         Mvua kiasi cha 850mm-1800mm kwa msimu
·         Udongo wenye PH kiasi cha 4.5-7.0
·         Joto liwe na 21centigrade-30centigrade
·         Mwinuko kutoka usawa wa bahari 0-2400m.

Mahindi pia hutumika katika Utengenezaji wa fueli; Mahindi pia hutumika kutengenezea fueli katika baadhi ya nchi tofauti tofauti kutoka kwenye mabaki yake ya mimea. Magunzi yake pia hutumika kama chanzo cha nishati. Mahindi hupatikana kwa urahisi, na kufanya upatikanaji wa nishati hiyo nyumbani kuwa rahisi zaidi

KUANDAASHAMBA, KUSAFISHA,  KULIMA/KUTIFUA
Ni vyema mashamba yaandaliwe mapema kabla ya msimu wa kupanda haujaanza ili kumpa mkulima fursa ya kupanda kwa wakati unaotakiwa.Kuna njia mbalimbali zinazotumika kuandaa mashamba. Kati ya njia hizi ni pamoja na kufyeka, kung’oa visiki na kulima. Shamba linaweza kulimwa kwa kutumia:
i). Jembe la mkono - wengi wanatumia
ii). Jembe la kukokotwa na wanyama kama ng’ombe
iii). Power tillers
iv). Matrekta
Matumizi ya trekta, power tillers na jembe la kukokotwa na wanyama yanapunguza nguvu kazi kwani vinachimbua udongo na kuufanya kuwa tifutifu (kufanya isiwe na mabonge makubwa, wala isiwe vumbi vumbi). Hii husaidia:
i). Mizizi ya mimea kupenyeza ardhini kirahisi
ii). Udongo kuweza kuhifadhi maji
iii). Udongo kuwa na hewa inayohitajika na mimea
iv). Ukuaji mzuri wa mimea hivyo kuongeza mavuno
ITAENDELEA


No comments:

Post a Comment