Thursday, 2 March 2017

CHANGAMOTO ZA UZALISHAJI WA UYOGA.

Katika maeneo mengi ambako tumefundisha uzalishaji wa uyoga uyoga kumekuwa na changamoto kadha wa kadha kamavile:
1Magonjwa ya uyoga.

magonjwa ya uyoga huweza kutokea tu endapo hali ya usafi na umakini kwa ujumla haujazingatiwa,kwa mfano kutochemsha au kutotumia dawa ya kuua wadudu hasa bacteria katika vimeng'enywa vinavotumika kuzalisha uyoga.
2. kuhalibika haraka.

kwa kawaida uyoga usipoyunzwa vema huweza kuhalibika kirahisi na hivo kuweza kumpa mkulima hasara.kuharibika husababishwa na visababishi kadhaa.

  • wadudu kama nzi weupe.kwa kwaida wadudu hawa huweza kutagia mayai kwenye uyoga na hatimaye kwa sababu ya ukuaji wa wadudu hao funza huweza kutokea.hivyo ili kuepuka tatizo hili tafadhali tumia nyavu nyeupe na ndogo kwenye chumba cha uzalishaji. 
  • joto la kuzidi .ili kuhifadhi vema ni vema ukahifadhi ndani ya jokofu au unaweza kujenga kibanda maalumu kwa ajili ya kuhifadhi mbogamboga,matunda na uyoga ambacho ni bora kuliko jokofu.
  • mda tangu uyoga uchumwe.ili uyoga uwe bora zaidi ni bora kuuvuna na kuuza au kuweza kutumia njia nyingine kama kuukausha au kuuoka.
  • uchukuaji au uhifadhi mbovu.chuma na weka kwenye chombo kikubwa ambacho huwezi kuukata kata.
  • aina ya uyoga.baadhi ya uyoga huweza kuvumilia kidogo zaidi ya mwingine,mfano ni pale unapokuta uyoga wa vinundu huweza kustahimili zaidi kuliko ule aina ya mamama(oyster).
 3.Upatikanaji wa mbegu za uyoga.Lakini kwa sasa chalajicomany limited tunalitatua tatizo hilo kwa wateja wetu wote.
4.soko.
Sisi kama CHALAJI COMPANY LIMITED tunatafuta masoko kwa wateja wetu waliojiunga kuwa washirika wetu.
JE UNAPENDA KUJUA NINI WASILIANA NASI.

No comments:

Post a Comment