Thursday, 2 March 2017

VIRUTUBISHO NDANI YA UYOGA

  • UYOGA nichanzo kizuri sana cha vitamini B (ikijumuisha riboflavini, niasini, na  pantotheniki asidi) ambazo husaidia kuto nguvu kwa kuvunja vunja protini,mafuta na wanga mwilini.vitamini B  pia ina kazi kubwa kwenye mfumo wa fahamu.
    • Pantotheniki asidi: husaidia katika uzalishaji wa homoni na pia husaidia katika mfumo wa fahamu. 
    • Riboflavini:husaidia kuweka afya ya seli nyekundu za damu 
    • Niasini:huwezesha afya ya ngozi na kuhakikisha mfumo wa mmeng'enyo wa chakula na ule wa fahamu vinafanya vizi vizuri (mujarabu) 
  • Uyoga pia ni chanzo kizuri cha madini mhimu mwilini mfano:
    • Seleniamu.  ni madini ambayo hufanya kazi kama antioksidanti ambayo huzuia seli za mwili kuharibiwa na ambayo isipokuwapo huweza kupelekea magonjwa ya moyo,baadhi ya aina za kansa na magonjwa ya kuzeeka kwa haraka. utafiti unaonesha kuwa madini haya ni mhimu sana hasa kama kinga mwili na kuongeza nguvu za kiume kwa wanaume
    • Ergothioneine :ni  madini yanayokuwepo kiasili ndani ya uyoga ambayo pamoja na mambo mengine huukinga mwili na maradhi mbalimbali. 
    • Coppa;Madini haya husaidia utengenezaji wa seli nyekundu za damu,hivyo ni mhimu sana kwa watoto,mama wajawazito na wagonjwa lakini ni mhimu sana pia kwa watu wote.madini haya pia husaidia kuweka mifupa kaika hali nzuri sana na kufanya mifumo ya fahamu kufanya vema. 
    • Potasiamu;ni madini ambayo kusawazisha majimaji mwilini na kuweka msawazo wa mdini katika mwili na hivyo kudhibiti mfumo shinikizo la damu.Pia inasaidia mfumo wa famu na misuli ukiwemo moyo kufanya kazi vema. Uyoga una  98-376 mg za potasiamu kwa gramu 84 za mlo ambazo ni sana na 3-11% mahataji ya potasiamu anayohita mtu kula kila siku.
  • Beta-glucans,husaidia sana kuamusha kinga mwili na kuzifanya kuwa uzo zaidi.
  • inavitamini D kwa wingi ambayo hupatikana kwenye kabeji na mwanga wa jua.

No comments:

Post a Comment