1.
UTANGULIZI.
Uyoga ni aina ya nyuzikuvu (fungus) yenye
kutofautiana na mimea mingine kwa kukosa chembechembe zinazowezesha mimea
kujitengenezea chakula yenyewe kwa kutumia hewa na mwanga. Uyoga unaota wenyewe
kwenye mashamba hasa wa katiwa mvua kwenye maeneo yenye mboji nyingi. Sasa hivi
nchini tunao utaalamu wakuotesha uyoga au ndani ya nyumba au nje kwe nye kivuli
maalumu.
1.1 HISTORIA
FUPI YA UYOGA.
Uyogaumefahamikanawanadamutanguenzizazamanisana.
Miaka elfunne kablayakuzaliwaKristo watu waliujua uyoga. Historia inatueleza
kwamba watu wameanza kulima kwa utaalamu mwaka 300 baada ya kuzaliwa Kristo.
Wadadisiwa mambo Waanauelezea Uyoga kufanana sana na chakula waisraeli.
walichokuwa wakila kule jangwani katika safari yao ya kutoka utumwani Misri.
Wakati Uyoga ukilimwa katika dunia yote, hapa
Afrika na hasa kwetu Tanzania mambo yalikuwa nitofauti kabisa.
Hakuna mtualiyesumbuka na kilimo hicho. Ni hapo majuzi tu mwaka 1993 ndipo ukulima ulianza Dar essalaam. Mwaka 1994 ukulima ulianza Arusha, mwaka 1995 ukulima ulianza hapa Mbeya.
Hakuna mtualiyesumbuka na kilimo hicho. Ni hapo majuzi tu mwaka 1993 ndipo ukulima ulianza Dar essalaam. Mwaka 1994 ukulima ulianza Arusha, mwaka 1995 ukulima ulianza hapa Mbeya.
2.0
AINA YA UYOGA.
2.1
Unaoliwa
na binadamu,baadhi ni
v Mamama(Oyster
mushroom).
v Uyogavifungu(Agaricusbitoquis)
v Kichwa
cha nyani (Monkey Head)
2.1.1 Uyoga ambao
unazalishwa kwa wingi sana hapa kwetu Tanzania
ni aina ya mamama kwa maana utaalamu unaohitajika siyo mgumu na kukubali
kuota vizuri ukiliganisha na aina nyingine ya uyoga.
3.0 FAIDA ZA UYOGA
Uyoga unamaajabu makubwa katika maisha ya mwanadamu,
Uyoga nilishe bora kwa mwanadamu, ni dawa na tiba kwa mwanadamu, ni zao la
kuingizia watu kipato, ni rafiki wa mazingira pia.
3.1 LISHE
v
Uyoga ni zao lenye viinilishe (amino acids) zote 22
zinazohitajika na mwili wa mwanadamu.
v
Protini iliyoko kwenye Uyoga inafikia kiwango
cha asilimia arobaini. Hii inalingana na protini iliyoko kwenye maziwa pamoja na
samaki
v
Kuna wingi mkubwa sana wa vitamini B,Cna D.
v
Uyoga hauna mafuta mengi. Unaasilimia tatu tu.Hivyo
hauna Colestrol.
v
Uyoga unayo madini yote muhimu kwa mwanadamu;
phosphorus, Iron, Calcium na Potash.
3.2TIBA
Utafiti uliofanyika siku za karibuni umethibitisha kuwepo
kwa dawa nyingi ndani ya uyoga zenye uwezo wa kutibu kwa ufanisi, magonjwa ya wanadamu
na mifugo. Kwa wanadamu magonjwa yafuatayo yanatibiwa:
3.2.1Uhongeza kinga mwilini hasa kwa wangonjwa wa HIV/AID
3.2.2Kisukari
3.2.3 Shinikizo la damu(B.P)
3.2.4 Uti wamgongo
3.2.5 Saratani
3.2.6 Matatizo yafigo
3.2.1Uhongeza kinga mwilini hasa kwa wangonjwa wa HIV/AID
3.2.2Kisukari
3.2.3 Shinikizo la damu(B.P)
3.2.4 Uti wamgongo
3.2.5 Saratani
3.2.6 Matatizo yafigo
Uyoga umeongeza ajira na kuinua kipato kwa rika zote kwa vijana pia kwa wazee katika kaya.
3.4 MBOLEA
Vimeng'enywa hivi hutumika kama mbolea shambani na katika bustani. Matokeo ya kutumia vimeng'enywa hivi yameonyesha ufanisi mkubwa.
3.5 NI LAISI KUZALISHA NA LINAITAJI LASIMALI NDOGO
Kilimo hiki huhitaji eneo dogo sana la ardhi pia huweza kuzalishwa na rika zote
4.0MAHITAJI YA UZALISHAJI WA UYOGA
4.1 Chumba
Kabla ya kuzalisha uyoga inabidi kuwa na chumba chenye paa ambalo litazuia jua, mvua na vumbi. Chumba hiki kinatakiwa kiwe na sakafu inayohifadhi unyevunyevu pamoja na sehemu ya giza na mwanga ambayo ni muhimu kwa kuotesha uyoga.
4.2Vimeng'enywe
4.2.1Vimeng’enywa
ni nini?
Ni
vile vitu vyote ambavyo ni chanzo cha virutubisho kwa uyoga.(chakula cha uyoga)
Mfano wa vimng’enywa ni,majani ya migomba, majani ya mahindi, majani ya karanga
na majani ya maharage. Kwa lugha rahisi ni vimeng’enywa ni mabaki ya mimea.
4.3Vibebeo(containers)
Ni
kama vile mifuko ya plastiki na ndoo zisizoshika kutu
4.4
Vichemshio
Pipa
tupu au sufuria kwa kuchemshia vimeng'enywa
4.5
Nishati
Inaweza
ikawa kuni, mkaa.
4.6
Maji
Kwa ajiri ya kuchemshia vimeng'enywa
4.7
MbeguMbegu za uyoga huzalishwa kwenye maabara zenye vifaa vinavyowezesha kuotesha mbegu hizo bila kuchafuliwa au kuchanganyika na vimelea kama bakteria, ukungu au jamii nyingine za uyoga ambazo haziliwi. Hapa Tanzania hivi sasa maabara hizo zipo Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kituo cha utafiti wa kilimo-Uyole, taasisi ya utafiti wa kilimo cha bustani- Tengeru (HORTI –Tengeru, Arusha), na TIRDO
4.8 Kamba
Kwa ajiri ya kufunga mifuko wakati wa kuchemsha
4.9 Kifaa chenye ncha
kali
Kama vile kisu, uma kwa ajiri ya kutoboa
mifuko iliyopandwa uyoga uweze kutoka4.9.1 Kichanja
Kwa hajiri ya kuteganisha maji na vimeng'enywa
5.0
HATUA ZA KUOTESHA UYOGA
5.1 Kusanya vimeng'enywaLoweka vimeng'enywa kwenye maji ya kawaida kwa muda wa siku nzima( saa 24)ili viweze kulainika
5.2 Funga kamba vibebeo
Kwa ajiri ya kuzuia backeria na hewa isingie kirahisi kwenye vimeng'enywa
5.3Chemsha vimeng'enywa
Kisha yachemshwe kwa muda wa dakika 20 kutegemeana chanzo chako cha nishati ili kuua vijidudu pamoja na vimelea vilivyomo.
5.4 Ipua vimeng'enywa
Ondoa vimeng'enywa vyako na kasha uviache vipoe kwa muda wa masaa 24 kutegemeana na aina ya vimeng'enywa
5.5Chukua vibebeo.
Kama vile rambo, ndoo zisizo shika kutu kirahisi kasha weka vimeng'enywa vilivyopoa, na funga kwa kamba.
5.6 Tia mbegu za uyoga
Tawanya mbengu za uyoga kwenye vibebeo ukiwa umevaa maski ili kuzuia backeria ukianzia chini kupanda, katikati na kumalizia juu kasha funga vizuri kibebeo chako.
5.7 Hifadhi kwenye giza
Weka mifuko kwenye chumba cha giza ili kuzuhia hewa ya oxgeni kuingia ndani, acha mifuko humo kwa muda wa siku 14-21 bila kufunua ili ukungu mweupe uweze kutanda vizuri.Utando wa uyoga ukishatanda vizuri kwenye mali ghafi ya kuoteshea, inaweza kuwekwa kwenye kichanja pia inaweza kuning'inizwa kwenye Kamba.
5.8
Ruhusu mwanga
Fungua madirisha ya chumba kwaajiri ya kuruhusu mwanga na hewa ya kutosha
kisichopigwa jua. Na kasha toboa mifuko ili kuruhusu uyonga uweze kutoka kiuraisi
na kutoa vichwa siku 2-3 baada ya kuwekwa kwenye mwanga kutokana na hali ya hewa
ya mahali husika.
7.0
UVUNAJI WA UYOGA
Uyoga huwa tayari kuvunwa kwa muda usiozidi sikutisini(90).Uyoga uvunwe kwa mkono
kwa kushika katikati ya shina la uyoga, kasha zungusha hadi uyoga ung'oke.Usiondoe
kichwa peke yake katika kuvuna uyoga kwa kubakiza shina huzuia uyoga mwingine kutokea.
Baada
ya kuvuna uyoga unaweza kuhifadhiwa kwa njia mbalimbali lakini njia inayopendekezwa
mara nyingi ni ile ya kuukausha uyoga kwa jua au joto la moto.au unaweza kuoka kwa
mafuta na baada ya hapo hifadhi katika mifuko na kupeleka sokoni.
No comments:
Post a Comment