Habari za siku ya leo ndugu msomaji.
leo tutaangalia umhimu wa tangawizi katka afya yako.
Faida za tangawizi ni pamoja na:
1. Inasaidia kuondoa kichefuchefu.
Kwa utafiti
uliofanyika uingereza kwa kuwashirikisha wajawazito 1278 na kugundua kuwa
tangawizi ilikuwa na uwezo wa kuondoa kichefuchefu na pia utafiti kama huo
ulifanyika katika chuo kikuu ch afya cha Rochester ulionyesha kuwa tangawizi
iliweza kuondoa kichefuchefu kwa wagonjwa waliokuwa wakipata matibabu ya mbalimbali. (1) (2)
2. Huweza kupambana na maambukizi ya fangasi.
Tangawizi ina kemikali inayoweza kupambana na fangasi wa aina
mbalimbali.mfano utafiti uliofanyika nchini Iran mwaka 2016 ulionyesha kuwa
tangawizi ilikuwa na uwezo wa kupambana na aina kadha ya fangasi wanaosababisha
magojwa ya midomo. (3),pia utafiti kwenye
mimea zaidi ya 29 uliweza kuonyesha kuwa tangawizi ilikuwa na uwezo wa kuua
kabisa fangasi. (4)
3. Huweza kuzuia vidonda vya tumbo
Tangawizi huweza kuzuia kutokea kwa vidonda vya tumbo kwa kisi
kikubwa kwa mfano ni ule utafiti uliofanyika mwaka 2011 ulinesha kwa tangawizi
ina uwezo mkubwa wa kuzuia chemicali za tumbo zinazoweza kusababisha vidonda
vya tumbo. (5)
4. Huweza kupunguza maumivu ya wakati wa
hedhi.
Wanawake wengi huweza kupata maumivu wakati wa hedhi
yakiambatana na maumivu ya kichwa,wengi hutumia dawa za madukani,lakini habari
njema ni kuwa tangawizi huweza kupunguza maumivu hayo na kufanya kipindi cha
hedhi yako kuwa murua.
Uchunguzi uliochapishwa kwenye jarida la “Alternative and
Complementary Medicine” (6) lilionyesha kuwa tangawizi ina uwezo wa kuondoa
maumivu ya wakati wa hedhi.
5. Huweza kuzuia kukua na kuopngezeka kwa seli
za kansa.
Uwepo wa chemikali ya 6-gingerol ambayo ni humhimu kwa ajili ya
kupambana na kansa.
6. Huweza kurekebisha kiwangao cha sukari mwilini.
Kwa wale wenye kisukari tangawizi ni mhimu sana kwa kurekebisha kiwango cha sukari katika mwili na kuweza kuzuia athari zaidi zinazo weza kutokea kama uharibifu wa mfumo wa fahamu unaoweza kuleta kiharusi na kuweza kuchelewa kupona kwa vidonda
7. Huweza kupunguza maumivu ya misuli.
Kwa sababu ya uwezo wake wa kupunguza uvimbe ,tangawizi kwa kuchanganya kwenye chakula huweza kupunguza maumivu ya mishipa na misuli.
8. Hupunguza kiwango cha mafuta mabaya (cholesterol)
mwilini.
Mafuta
mabaya mwilini huweza kusababisha matatizo ya moyo na shinikizo la damu,kwa
kuweza kutumia tangawizi, ni rahisi kupunguza lehemu na kuepukana na athali
zinazoweza kuambatana na magonjwa hayo.
9. Ina uwezo wa kurekebisha mfumo wa ubongo.
Utafiti
uliofanyika mwaka 2012 uliweza kuonyesha kuwa watumiaji wa tangawizi huwa na
uwezekano mdogo wa magonjwa ya akili,kuzeeka kwa ubongo nk.
Faida zngine ni
pamoja na kupambana na magonjwa ya bacteria,kuweza
kupunguza uvimbe pia husaidia kuwezesha umeng’enyaji mzuri wa chakula..
No comments:
Post a Comment