Wednesday, 1 March 2017

MWENDELEZO KILIMO BORA CHA MAHINDI

KANUNI ZA KILIMO CHA MAHINDI
1.    PANDA MAPEMA;
Tayarisha shamba mapema kwa zana yoyote iliyo ndani ya uwezo wako (jembe, maksai, trekta) Kwa maeneo mengi ya hapa Tanzania Panda kuanzia tarehe15 Novemba hadi kati kati ya mwezi Desemba.
Upandaji wa mahindi unatakiwa ufanyike pale tu mvua zinapoanza kunyesha, kuchelewa kupanda mahindi kwa siku moja hupunguza uzalishaji wa mmea kwa asilimia 1 hadi 2. Kupanda mbegu za mahindi katika hecta moja kwa mkono kunahitaji angalau siku tano hadi kumi. Mbegu huwekwa kwenye shimo lenye urefu wa sentimita tano ili kuzuia kuchipua kutokana na mvua zisizo za kweli. Kwa ekari moja kilo 8 hadi 10 za mbegu za mahindi zitahitajika na kilo 25 kwa hecta.
Ili kuwa na mahindi yaliyosimama vizuri, inashauriwa kuacha nafasi ya sentimita
75 (mstari kwa mstari) na sentimita 30 (mbegu kwa mbegu) ambazo zitatoa mazao ya mahindi 44,000 kwa hecta moja katika maeneo yenye mvua za kutosha. Au unaweza kuweka nafasi ya 75×25 ambayo itatoa mimea 53,000 kwa hecta moja. Katika maeneo ambayo ni makavu sana inashauriwa kuongeza ukubwa wa nafasi hadi angalau 90×30.
>Aina za nafasi za upandaji zinatofautiana kutokana na
>Mbolea katika ardhi husika
>Kiasi cha mvua kinachopatikana kwa msimu
>Uwezekano wa kumudu kuhudumia (mfano kupalilia)
>Aina ya mbegu
>Matumizi ya mahindi (biashara au chakula)

Matatizo yanayoweza kujitokeza ukichelewa kupanda mahindi
o  Kupungua kwa mazao
o  Kushambuliwa na wadudu
o  Kukauka kwa mazao (endapo mvua zitakua zimepungua)

2.    TUMIA MBEGU BORA
Mbegu bora; Matumizi ya mbegu bora ni muhimu katika upatikanaji wa mavuno mengi na bora. Kuna makundi mawili makuu ya mbegu ambayo ni:
i). Mbegu za asili: Ni zile ambazo zimetumika miaka mingi katika historia ya kilimo
ii). Mbegu zilizoboreshwa: Hizi ni zile zilizoboreshwa kutoka mbegu za asili. Kundi hili linagawanywa kwenye makundi mawili - composite varieties na mbegu chotara (Hybrids). Ushauri wa matumizi ya mbegu zilizoboreshwa unatofautiana kutoka eneo moja na lingine kwa
sababu ya:
i). Mwinuko kutoka usawa wa bahari
ii). Kiasi cha mvua katika eneo husika
iii). Muda unaotumia mbegu hadi kukomaa
Mbegu za mahindi zilizoboreshwa ni kama TMV1, TAN 250, TAN 254, Staha, kilima st, Situka na zingine zote zinazoanza na herufi “H” kama vile H 250, H 251 na H 615.

ZIFUATAZO NI MBEGU PAMOJA NA VIPIMO VYAKE KATIKA UPANDAJI NA UZALISHAJI WAKE
       I.            KILIMA ST.
Mwinuko kutoka usawa wa bahari kati ya 900-1500m.
Kukomaa ni baada ya siku 135-140
Inazalisha tani 5 hadi 6 kwa hekari
Nafasi katika upandaji
90cm x 25cm mbegu moja kwa shimo (mimea 44,000 kwa hekari)
90cm x 50cm mbegu mbili kwa shimo
75cm x 30cm mbegu moja kwa shimo
75cm x 60cm mbegu mbili kwa shimo (mimea 44,000 kwa hekari)

    II.            TMV-1
Mwinuko kutoka usawawa bahari chini ya 1500m.
Kukomaa ni baada ya siku 110-115
Inazalisha tani 4 hadi 4.5 kwa hekari
Nafasi katika upandaji
90cmx 25cm mbegu moja kwa shimo (mimea 44,000 kwa hekari)
90cm x 50cm mbegu mbili kwa shimo
75cm x 30cm mbegu moja kwa shimo
75cm x 60cm mbegu mbili kwa shimo (mimea 44,000 kwa hekari)

 III.            TMV-2
Mwinuko kutoka usawawa bahari chini ya 1500m.
Kukomaa ni baada ya siku 180-190
Inazalisha tani 7 kwa hekari
Nafasi katika upandaji
90cm x 45cm mbegu moja kwa shimo
75cm x 30cm mbegu moja kwa shimo (mimea 44,000 kwa hekari)
90cm x 50cm au 75cm x 60cm mbegu mbili kwa shimo

 IV.            TUXPENO
Mwinuko kutoka usawa wa bahari 0-900m.
Kukomaa ni baada ya siku 120-130
Inazalisha tani 3-4 kwa hekari
Nafasi katika upandaji
90cm x 25cm mbegu moja kwa shimo
75cm x 30cm mbegu moja kwa shimo (mimea 44,000 kwa hekari)
90cm x 50cm au 75cm x 60cm mbegu mbili kwa shimo

    V.            KATUMANI
Mwinuko kutoka usawa wa bahari chini ya 1500m.
Kukomaa ni baada ya siku 90
Inazalisha tani 3-4 kwa hekari
Nafasi katika upandaji
60cm x 30cm mbegu moja kwa shimo (mimea 55,000 kwa heakari)

 VI.            KITO
Mwinuko kutoka usawa wa bahari 0-1300m.
Kukomaa ni baada ya siku 90
Inazalisha tani 2-3 kwa hekari
Nafasi katika upandaji
60cm x 30cm mbegu moja kwa shimo (mimea 55,000 kwa heakari)
VII.            STAHA
Mwinuko kutoka usawa wa bahari 0-900m.
Kukomaa ni baada ya siku 120
Inazalisha tani 4-5 kwa hekari
Nafasi katika upandaji
90cm x 25cm mbegu moja kwa shimo
75cm x 30cm mbegu moja kwa shimo (mimea 44,000 kwa hekari)
90cm x 50cm au 75cm x 60cm mbegu mbili kwa shimo

3.    TUMIA MBOLEA.
Samadi/mboji: Tani 5-8 kwa ekari.
Changanya na mfuko 1 wa TSP kwa ekari. Weka mbolea kwenye shimo la kupandia au rutubisha shamba zima kwa kuifukia kwa jembe la mkono, maksai au trekta kabla ya kupanda.
Mbolea za chumvi chumvi.
Mtiririko huu unaonyesha matumizi ya Nitrogen inayohitajika wakati wa kupanda na wakati wa kukuzia.
Sehemu zenye mvua nyingi (mm 750 au zaidi)
-SA mfuko 1 na nusu kupandia, mifuko 3 kukuzia.
-CAN mfuko 1 kupandia, mifuko 2 na nusu kukuzia.
-UREA mfuko 1  kupandia, mfuko 1 na nusu kukuzia.
-DAP mfuko 1 kupandia, SA 4, au CAN 3 au Urea 2 kukuzia.

Maeneo yenye mvua haba (mm550-750)
-SA 1 kupandia, mifuko 2 kukuzia.
-CAN 1 kupandia, mfuko 1 na nusu kukuzia.
-UREA nusu mfuko kupandia, mfuko 1 na nusu kukuzia.
-DAP 1 kupandia, SA 4 NA nusu au CAN 3 au Urea 1 kukuzia.
Katika maeneo yenye mvua chini ya mm 550 kwa msimu ni lazima umwagiliaji ufanyik

JINSI YA KUWEKA MBOLEA ZA KUPANDIA
Mbolea hizi zinawekwa shambani kabla ya kupanda/kusia mbegu. Zinawekwa kwa njia mbalimbali kama vile kusambaza kwenye eneo husika na kuchanganya na udongo, au kuweka kwenye mistari au mashimo ya kupandia. Ni bora zaidi kuchanganya mbolea za Minjigu Phosphate au Minjingu Mazao na udongo kuliko kutia kwenye shimo la kupandia. Pia kuchanganya mbolea na udongo huondoa athari za mbolea kwenye uotaji wa mbegu, hasa kama kuna uhaba wa unyevunyevu.
Viwango vya mbolea za kupandia
Kiwango cha mbolea za kupandia kilichopendekezwa ni kilo 20 fosfati (P) kwa hektari ambayo ni sawasawa na kiasi cha aina mbambali za mbolea za kupandia kama inavyoonyeshwa kwenye jedwali
Jedwali na. 1: Kiasi cha mbolea za kupandia kwa inayopendekezwa kwa eneo (hektari au ekari)
Aina ya mbolea za 
kupandia
Idadi ya mifuko ya kilo 50 kwa hektari
Idadi ya mifuko ya kilo 50 kwa ekari
Viwango kwa kila shimo
DAP
2
1
Nusu kizibo cha soda
Minjingu fosfati
3
Kizibo kimoja cha soda
Minjingu Mazao
2
Kizibo kimoja na nusu cha soda

MUDA WA KUPANDA
Muda wa kupanda unatofautiana kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na majira ya mvua. Kwa mfano katika wilaya ya Morogoro tarehe za kupanda ni kuanzia februari 15 hadi Machi 15. Mkulima anashauriwa afuate kalenda ya muda wa kupanda kama anavyoshauriwa na bwana shamba wake.

4.    PANDA KWA NAFASI
Kupanda kwa nafasi ni kati ya njia bora za kilimo inayomwezesha mkulima kupata mazao bora. Hivyo ni muhimu sana kuzingatia kupanda kwa mistari na kufuata nafasi zinazoshauriwa na wataalamu wa kilimo. Kwa mfano nafasi zifuatazo zinaweza kutumika katika upandaji wa mahindi:
Nafasi
Idadi ya mbegu kwa kila shimo
Kiwango cha mbolea kutumia kizibo cha chupa
90 sm X 30 sm
1
1
90 sm X 25 sm
1
1
90 sm X 50 sm
2
2

1.    PALILIA VIZURI
Palilia vizuri.Palilia mahindi mara 2 au 3, palizi ya kwanza iwe wiki 2-3 baada ya mbegu kuchipua. ya pili au tatu baada ya mbegu kuchanua. Uzaaji hauongezeki ukipalilia baada ya mhindi kuchanua. Kwa wenye uwezo zipo dawa za kuua magugu (mfano PRIMAGRAM, ATRANEX, GESAPRIM, GRAMAXONE, ROUNDUP nk)
Ni muhimu shamba lipaliliwe baada ya mimea kuota ili kuondoa magugu. Magugu ni mimea hivyo hushindana na mimea iliyopandwa na mkulima kwa kunyonya virutubisho ardhini. Magugu yanaweza pia kuhifadhi wadudu na magonjwa yanayoweza kushambulia mimea iliyopandwa na hivyo
kupunguza mavuno.Magugu Kupalilia mahindi kunatakiwa kufanyike wiki 4 hadi 6 za mwazo baada ya kujitokeza kwani magugu husababisha uharibifu mkubwa katika mahindi kwa kuchukua virutubisho ambavyo vingetumika kama chakula cha mmea.

2.    ZUIA WADUDU WAHARIBIFU (HASA BUNGUA);
Nyunyizia dawa kwenye majani ya mahindi yakiwa na urefu wa sm75, rudia baadae ukiona mashambulizi.

Dawa za viwandani: Actellic, Thionex, Endosulfan, Dursban, Karate, Dimepaz 40 na nyinginezo.Kipimo: mls 30 kwa lita 15 za maji.Dawa za asili: kwa mfano utupa, dawa hizi hazina kiwango maalumu. NB: Mbegu bora za mahindi zina uwezo wakustahimili magonjwa ya mahindi
ITAENDELEA

No comments:

Post a Comment