UTANGULIZI:
Viazi
mviringi ni zao muhimu la chakula. Tanzania viazi mvringo husitawi zaidi katika
sehemu za miinuko ambazo zina mvua nyingi na baridi kali.
UMUHIMU WA VIAZI MVIRINGO/MATUMIZI:
Viazi
mviringo vina asilimia kubwa ya chakula chenye asili ya wanga. Viini kama vile
vya protini, madini, vitamini na maji. Hivi vyote hutosheleza mahitaji ya mwili
wa binadamu. Pia viazi mviringo hutumika kama zao la biashara kuweza kumpatia
mkulima ffedhaza kujikimu na mahitaji mengineyo katika familia.Ili mkulima
aweze kulima na kuzalisha kwa tija mbegu bora na kupata mavuno mengi, ni lazima
afuate kanuni bora za uzalishaji wa zao la viazi.
ü Hali
ya hewa kwa zao la viazi
ü Hali
na aina ya udongo
ü Virutubisho
ndani ya udongo
ü Magonjwa
na wadudu
ü Namna
ya kuvuna na kuhifadhi mbegu na viazi vya chakula.
ü Ujenzi
wa maghala ya kuhifadhia mbegu na viazi vya chakula.
Kijitabu
hiki kinaelezea kanuni bora za uzalishaji wa zao la viazi mviringo. Mkulima
anashauriwa kukisoma kwa makini, ili aweze kujua kwa undani hasa kwa wakulima
wanao jianda kuingia katika biashara ya uzalishaji wa mbegu za viazi mviringo.
KANUNI
ZA UZALISHAJI BORA WA MBEGU NA VIAZI VYA CHAKULA
1. Uchaguzi wa shamba
Kwa ajili ya uzalishaji bora na wenye
tija, lazima mkulima afahamu mambo mbalimbali yahusuyo kanuni za kilimo bora.
Mija ya mambo muhimi ni uwezo wa mkulima kuweza kuchagua eneo zuri la kulima
viazi mviringo, liwe kwa ajili ya mbegu au viazi vya chakula. Kuna utofauti wa
eneo la viazi vya chakula na viazi vya mbegu.
Kwa ujumla viazi mviringo huhitaji
mwanga wa jua wa kutosha, Udongo wenye rutuba, na usiokuwa na tindikali nyingi.
Pia udongo unatakiwa ule usio twamisha maji, udongo laini, kwani udongo ukiwa
mgumu, hali hii husababisha viazi kuwa na mwonekano wa tofauti au kutokuwa na
ukubwa unaotakiwa.
Wakati wa kuchagua mashamba kwa ajili ya
uzalishaji viazi, mkulima anashauriwa kuangalia yafuatayo;-
v Shamba
lisiwe kwenye mteremko mkali, hii ni kwasababu wakati wa kuvuna inakuwa kazi
kubeba viazi kutoka bondeni, na hata hivyo wakati wa mvua nyingi maji yanaweza
kuharibu mazao na kuondoa virutubisho.
v Historia
ya shamba- Ni vizuri kabla ya mkulima wa mbegu za viazi hajapanda, ajue taarifa
za shamba hilo, hasa aina ya mazao yaliyopandwa msimu uliopita na historia ya
magonjwa. Kwa ujumla shamba linatakiwa lisiwe na historia ya magonjwa kama ya
Mnyauko bacteria, virusi, au kuwa na wadudu kama minyoo fundo au wadudu nondo
wa viazi. Hali hii itasababisha mbegu kukosa ubora na hata kupunguza mavuno kwa
mkulima.
Mahitaji
ya viazi mviringo
Ili viazi ziweze kumea na kustawi,
vinahitaji mazingira na hali ya hewa nzuri inayoruhusu viazi kustawi. Kimsingi
viazi zinahitaji hali ya ubaridi na miinuko ya kuanzia erefu wa mita 800 mpaka
3000 kutoka usawa wa bahari. Hata hivyo kwa wakulima wa mbegu, wanatakiwa kuwa
na mashamba ya mbegu sehemu zenye miinuko ya juu, ili kuepuka na milipuko ya
magonjwa yanayo weza kushambulia na kuharibu mbegu za viazi. Viazi vinahitaji
joto la wastani kuanzia 10-220C. Pia viazi vinahitaji angalau masaa
12 ya mwanga ili viweze kustawi vizuri shambani na kuleta mavuno yenye tija.
Udongo unaofaa unatakiwa uwe wenye tindikali ndogo kuanzia 5.0-5.5, hivyo mkulima anashauriwa kufanya uchunguzi
wa hali ya tindikali ya udongo kabla ya kupanda. Tindikali ya udongo ikizidi
kiwango cha kitaalam, husababisha mazao kushindwa kupata virutubisho kutoka
kwenye udongo.
Jinsi
ya kutayarisha shamba
Kwa mkulima yeyote, zoezi hili ni la
kawaida sana. Ili kupata mavuno yenye tija, mkulima hana budi kujua jinsi gani
atayarishe shamba lake, tayari kwa kupanda viazi. Shamba la kupanda viazi
linahitaji kulimwa kwa makini na kuhakikisha udongo umekuwa laini wenye
kuruhusu viazi kuota kwa urahisi. Kwa wakulima wenye uwezo wanaweza kutumia
trekta au jembe la kukokotwa na ng’ombe. Wakulima walio wengi wanatumia majembe
ya mkono, hivyo anatakiwa kuhakikisha jembe lake linaingia chini sana ili
kuweza kulainisha udongo.
Wakati wakuandaa shamba ndiyo muda mzuri
wa kuondoa matakataka yote ili shamba libaki safi na salama kwa ajili ya
kupanda mbegu za viazi. Faida za kutifua udongo vizuri kabla ya kupanda ni
pamoja na kuongeza rutuba ya udongo, kupunguza uotaji wa magugu. Husaidia
kuweka juu ya udongo vimelea vya magonjwa na wadudu hali inayosababisha wapigwe
na jua kisha kufa.
Jinsi
ya Kupanda
Muda mzuri kwa mkulima kupanda mbegu za
viazi ni mara tu mvua za mwanzo zinapoanza kunyesha, na hali ya unyevunyevu
kuwa ya kutosha kwenye udongo. Vile vile ni jambo la msingi kupanda kwa
kuangalia majira, ili mimea isije ikakumbana na hali ya hewa inayoruhusu
kustawi kwa mimea, mfano kipindi chenye baridi sana au joto sana au ukame, pia
kuwepo na magonjwa na wadudu wasumbufu wa viazi. Hivyo mkulima anashauriwa
kujua majira mazuri ya kuweza kupanda viazi. Kipindi kibaya kwa mazao ya viazi
ni hatua ya mimea ya viazi inapokaribia kuchanua, hiki kipindi, mimea ya viazi
haihitaji mvua nyingi, au hali ya ukame. Mkulima anashauriwa kupanda kwa matuta
mara tu baada ya kufukia mbegu ardhini. Matuta yana faidi nyingi sana, kwanza
yanazuia mbolea iliyowekwa isipotelee au kubebwa na maji pindi mvua
inaponyesha, yanapunguza uotaji wa magugu shambani, yanarahisisha wakati wa
palizi, yanasaidia kutunza unyevuunyevu, na pia yanapunguza wadudu nondo kuingia
ndani ya viazi.
Nafasi
ya kupanda
Kwa
kawaida ili mkulima aweze kupata mavuno mengi, ni lazima azingatie nafasi ya
upandaji. Kwa upande wa viazi kuna nafasi za aina mbalimbali kutegemea na lengo
la mkulima pamija na aina ya mbegu za viazi. Kuna nafasi kwa ajili ya kulima
viazi vya chakula na nafasi ya kupanda kwa ajili ya wakulima wanao lima mbegu
za viazi. Nafasi ya kupanda ina mchango mkubwa kwenye mavuno ya viazi, hasa
ukubwa wa kiazi chenyewe. Nafasi ya kupanda iliyoshauliwa kwa wakulima wa viazi
vya chakula ni sentimita 75 au 80
mstari hadi mstari na sentimita 30
kiazi hadi kiazi. Nafasi hii huruhusu ukuaji mzuri na kuwa na saizi nzuri ya
viazi kwa ajili ya chakula. Pia nafasi hii mkulima anatakiwa kuwa na mbegu za
viazi zisizopungua 44,440 au 41,140 kwa hekta. Nafasi kwa ajili ya
uzalishaji wa mbegu za viazi hutofautiana na nafasi ya uzalishaji wa viazi vya
chakula. Kwa upande wa viazi vya mbegu nafasi ya kupanda ni Kati ya mmea na
mmea ni sm 25 au sm 30 na
Kati ya mstari na mstari ni sm 70. Hii husaidia kutengeneza viazi vyenye
ukubwa mdogo ukilinganisha na viazi vya chakula. Mkulima anatakiwa kuzingatia
nafasi hizi ili mbegu itakayozalishwa iwe na ukubwa unaofaa kwa mbegu. Mkulima
atahitaji kiasi cha mbegu kati ya 57,140 au 47,620kwa hekta.
AINA NA UKUBWA WA MBEGU
Hili jambo la muhimu sana
kwa mkulima kutambua ni aina gani ya mbegu anatakiwa kupanda na ina patikana
wapi. Pia ni muhimu kujua hata ni ukubwa gani wa mbegu za viazi unafaa kutumika
kupanda. Wakulima baadhi hupanda mbegu za viazi zilizo katwa vipande vipande,
na wengine hutumia kiazi kizima lakini vidongo. Kitaalam inashauri mbegu ya
viazi iliyosahihi kwa kupandwa haitakiwi kukatwa vipande vipande, hali hii
husababisha mwanya wa wadudu na magonjwa kuingia na kushambulia mbegu mara
baada ya kupanda. Mbegu inatakiwa kuwa
nzima, na yenye ukubwa wa saizi ya yai la kuku (28-35milimita).
SIFA ZA MBEGU BORA ZA VIAZI MVIRINGO
Mbegu bora ya viazi mviringo
inatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:-
1.
Aina inayotambulika na isiyochanganyika na aina
yoyote
2.
Isiyokuwa na magonjwa au wadudu wa aina yoyote
3.
Iwe imepitia hatua zote za kuwa mbegu
4.
Isiwe na michubuko au kidonda
5.
Iwe na ukubwa unaokubalika
6.
Iwe imechipua na kuwa na machipukizi yenye afya
IITAENDELEA,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
No comments:
Post a Comment