FAIDA
ZA KITUNGUU SAUMU.
Kitunguu saumu kina manufaa makubwa
katika mwili wa binadamu, kiasi kwamba ni rafiki mkubwa wa moyo,mbali na
kuusaidia moyo usikumbwe na maradhi, kitunguu saumu pia kinazuia saratani ,
huingizwa oksijeni inapotakiwa , hupunguza shinikizo la damu na kolestrol,
hupambana na septini, bacteria, kuganda damu na ute. Kiungo hicho cha chakula
huhami mwili dhidi ya utitiri wa vimelea
na bacteria, fangasi na maambukizi ya virusi vingine. Pia huimarisha mishipa ya
moyo na damu na husaidia kuzuia shambulizi la ugonjwa wa saratani. Kitunguu
saumu ni moja ya viungo asilia vinavyotia msukumo zaidi wakati wa uzalishaji wa
chembechembe nyeupe za damu.
Aina
za vitunguu saumu maarufu kwa matumizi ya kawaida ni tatu,
1. SOFT NECK (ngozi nyororo)
- ni nyeupe huzaa kwa muda mfupi.
2. SILVER SKIN(ngozi ya fedha)-
vina rangi ya silver vikikaushwa vinaweza kukaa hadi mwaka mmoja.
3. ANTICHOKE - vina rangi
nyekundu kwa mbali.
katika nchi yetu ya tanzania vinapatikana vitunguu swaumu ya aina tatu
1. Kitunguu saumu chenye mafuta makali.
2. Kitunguu saumu chenye madini ya protini
3. kitunguu saumu chenye madini, protini na mafuta mepesi.
Hiki ndicho tulacho kila siku hapa kwetu na wengi hutumia kama dawa wakati hakina sifa za kuwa dawa
1. Kitunguu saumu chenye mafuta makali.
2. Kitunguu saumu chenye madini ya protini
3. kitunguu saumu chenye madini, protini na mafuta mepesi.
Hiki ndicho tulacho kila siku hapa kwetu na wengi hutumia kama dawa wakati hakina sifa za kuwa dawa
Udongo
Kitunguu saumu huota zaidi ukanda wa
juu kuanzia mita 900 hadi 1500. Pia huota katika udongo wa aina yeyote lakini
hustawi zaidi katika udongo usiotuamisha maji. Udongo huo ni lazima uwe na
mbolea ya kutosha hasa ya asili.
Ikiwa udongo wako ama ardhi
unayotumia kuotesha kitunguu chako haina mbolea ya kutosha basi hakikisha
unaurutubisha kwa kuweka mboji ama samadi iliyoozeshwa vizuri. Pia waweza
kuweka samadi mbichi iliyotoka moja kwa moja zizini katika shamba lako kisha
kulilima huku ukichanganya samadi na udongo vizuri na kuliacha kwa muda wa
miezi saba hadi kumi kisha kulilima tena na kuotesha vitunguu vyako.
Mbolea za viwandani kama Ammonium
Sulphate, Ammonium Nitrate, DAP, Urea na nyingine zaweza kutumika kwa kiwango
kitakachoshauriwa na wataalamu wa kilimo na kwa muda sahihi japo hatukushauri
sana kuitumia kwani mbolea ya samadi pekee yatosha.
Hali
ya hewa
Kwa
nchi ya Tanzania, zao hili huoteshwa na kustawi vizuri katika kipindi ambacho
joto ama ni la wastani. Iwe ni kipindi cha baridi japo si baridi sana (Nyuzi
joto 18C hadi 22C).
Utayarishaji
wa shamba
Hakikisha
shamba lako lipo katika eneo zuri lisilotuamisha maji na lisafishe vizuri kwa
kuondoa magugu yote na kisha kuyafukia kwani ni rutuba pindi yakioza. Weka
mboji na kisha lilime vizuri kwa kuchanganya mbole na udongo tayari kwa
kuotesha.
Utayarishaji
wa mbegu
Vitunguu
vinavyoota vizuri ni vile vilivyohifadhiwa sehemu nzuri isiyokuwa na unyevu, na
katika eneo lenye joto la wastani. Kama utahifadhi katika sehemu yenye joto
jingi na hakuna hewa ya kutosha basi ukiviotesha vitunguu hivyo vitazalisha
mavuno duni na dhaifu.
Kabla
ya kupeleka shambani, chukua kitunguu saumu na kuchambua kwa kutenganisha
vitunguu kimoja kimoja kisha kuchagua vile vitunguu vikubwa kwa kuwa hivi
ndivyo vitakavyokupatia mavuno mengi na vitunguu vyenye ubora, kisha peleka
shambani tayari kwa kuotesha.
Namna
ya kuotesha
Piga
mashimo kama ya kuoteshea maharage. Nafasi kati ya mche na mche iwe ni
sentimeta 8-12 na kati ya mstari na mstari iwe ni sentimeta 25-30 (visiwe
mbalimbali kama kitunguu maji kwani vitunguu swaumu havinenepi sana na
unapootesha karibu ndipo unapokuwa na kiwango kikubwa cha mavuno.
Weka
kitunguu chako katika mashimo ukihakikisha kuwa mizizi inakuwa chini na shina
linaangalia juu. Hakikisha vitunguu vyako haviegemei upande wowote bali
vimesimama wima.
Baada
ya kuweka katika mashimo, fukia kwa udongo wa kutosha na uukandamize kwa nguvu
kiasi ili kuhakikisha kitunguu chako kimekaa vizuri na hakiwezi kuanguka ama
kuathiriwa na kitu chochote kama kung’olewa na mvua au maji wakati wa
kumwagilia. Pia kwa kufanya hivyo utakinga mazao yako kuharibiwa na wanyama
kama mbwa wakati wakikatisha na hata kuingia katika shamba lako.
Kuchipua
Baada
ya siku kumi hadi siku kumi na sita, kitunguu swaumu kitachipua na kuanza kutoa
majani hadi kumi na sita. Jani la katikati ambalo litaweka mbegu, litaendelea
kukua na kupita majani mengine kwa urefu (mbegu hiyo ni kitunguu na huwa ni
kimoja tu, lakini utakapokiotesha baada ya kuvuna kitaota na kuzaa vitunguu
vingine vingi).
Umwagiliaji
Kwa
kipindi cha mvua, huna haja kabisa kumwagilia kwani maji ya mvua tayari
yanatosha. Kama ni kipindi cha kiangazi hakikisha unamwagilia vitunguu vyako
kila unapoona shamba limekauka. Unaweza kumwagilia mara mbili hadi tatu kwa
wiki.
Usimwagilie
vitunguu wakati wa mchana au jioni. Ni vizuri sana kumwagilia wakati wa asubuhi
ili kuipa uwezo wa kupambana na magonjwa kwani wakati kama wa jioni utaongeza
uwezo wa vitunguu kushambuliwa na barafu na hata kuoza.
Uwe
na utaratibu wa kuchunguza vitunguu vyako kama vimezaliana vya kutosha hasa
baada ya miezi miwili kwa kuchimba kidogo. Ukishagundua kuwa vimezaliana
vizuri, usimwagilie tena bali viache na kuvipa nafasi ya kukomaa, kwani
ukiendelea na umwagiliaji basi vitunguu vyako vitaoza.
Usafi
wa shamba
Mara
zote shamba lako linahitajika kuwa safi kwa kilimo bora. Hakikisha unafanya
usafi kwa kung’oa magugu na majani yasiyohitajika ili kuondoa ushindani baina
yake na vitunguu vyako ambavyo vitakuwa vikigombea rutuba, hewa na maji.
Ni
muhimu sana kufanya palizi walau mara nne hadi tano kufikia mavuno.
Kama
ilivyo kwa mazao mengi ya bustani, kitunguu saumu hushambuliwa na magonjwa kama
ukungu, kuoza, fangas pamoja na wadudu.
Namna
ya kuondokana na magonjwa hayo
Ni
muhimu sana kudhibiti magonjwa haya mara tu uonapo dalili kwa kutumia
viuatilifu ili kuondokana na hasara kubwa itakayotokea.
Unatakiwa
pia kufanya kilimo cha mzunguko wa mazao katika shamba lako yasiyo jamii moja
ya vitunguu saumu kama kuotesha mahindi, maharage ili kuondokana na magonjwa
mengine ambayo yanaweza kuwa sugu.
Pia,
kuepukana na umwagiliaji wa jioni na usiku pamoja na kuotesha katika maeneo
yanayotuamisha maji kutasaidia kuzuia ugonjwa wa kutu kwenye majani na fangas.
Ikiwa
mimea tayari imevamiwa na ugonjwa wa kutu, basi mimea yote ing’olewe na
kuchomwa ili kuikinga mimea ijayo itakayooteshwa katika shamba hilo.
Kukomaa
hadi kuvuna
Kitunguu
saumu huchukua miezi mitatu na nusu hadi minne kukomaa. Utagundua kuwa kitunguu
chako kimekomaa na kipo tayari kuvunwa mara baada ya jani lake dogo la mwisho
litakapokauka. Hapo utatakiwa kuingia shambani na kuvuna.
Namna ya kuhifadhi
Mara
baada ya kuving’oa vitunguu vyako, na majani yake yakiwa bado mabichi, chukua
kamba na funga mafundo ya ukubwa kiasi (Unafunga kwenye majani), kisha
vining’inize juu katika eneo lenye joto la wastani (kusiwe na unyevu wala
ubaridi). Vitunguu vyako vitaendelea kukauka taratibu huku vikinyonya yale maji
yote yaliyopo kwenye majani yake.
Pia
waweza kuvikata majani na kupunguza mizizi baada ya kung’oa kisha kuweka darini
na vitaendelea kukauka taratibu.
Kama
ulitumia mbolea ya samadi au mboji, waweza kuhifadhi kitunguu chako kwa muda wa
miezi saba hadi nane bila kuharibika na ikiwa umetumia mbolea za viwandani basi
vitunguu vyako vyaweza kuharibika baada ya miezi mitatu au minne.
Faida
za kitunguu saumu kiafya
Kutokana
na tafiti mbalimbali zilizofanywa na wanasayansi kama Louis Pasteur, kitunguu saumu kimegundulika kuwa na uwezo wa kutibu na kukinga
magonjwa mengi yanayomsumbua binadamu kila wakati.
Imegundulika
kuwa kitunguu saumu husaidia kuzuia maradhi ya saratani pamoja na malaria
kutokana na kemikali ambazo hutoka baada ya kukata ama wakati wa kutafuna.
Uchunguzi
umebaini kuwa kitunguu saumu huweza kupunguza athari za kemikali nyingine
zisizofaa mwilini hasa zitokanazo na moshi na kuimarisha uwezo wa seli za
mwili.
Mwaka
1845, mwanasayansi Pasteur aligundua kuwa kitunguu swaumu huweza kutumika kama
tiba ya vidonda na huzuia donda ndugu kwa kiasi kikubwa.
Haikuishia
hapo, kitunguu saumu pia hutumika kama tiba ya mafua, kuzuia magonjwa ya moyo
kwa kupungua kiwango cha lijamu, kupunguza shinikizo la damu na kurekebisha
kiwango cha sukari mwilini.
Jinsi gani naweza kupata mbegu? Na mbegu ya bei gani yaweza kutosha kwa hekari moja? Na gharama hadi kuvuna niNkiasi Gani na faida ki fedha ikoje?
ReplyDeleteHapa kuhusu miezi ya kupanda mpaka mavuno sio kweli.kwani ni michache mno kwa mkulima ninae lima huchukua miezi sita paka saba kufika kuvunwa,maelezo mengne yako sahihi yatamsaidia mkulima anaenza kulima hili zao
ReplyDeleteGharama ya uzalishaj inafaa niwe na kias gn
DeleteMkuu vitunguu swaum vinastawi sana mkoa gani?
DeleteGunia tano naweza tunzaje?
ReplyDeleteJe ni muda gani unatumika mpaka kuvuna maana nakala zingine zinasema miezi sita Hadi saba zingine zinasema miezi mitatu Hadi mitano
ReplyDeleteAsante
ReplyDeleteAsante
ReplyDeleteNataraji kulima zao hili je? naipataje mbegu,kiasi ekali moja,makisio ya gharama je ikoje kwa mlio lima
ReplyDelete