ORODHA YA MAJEDWALI.
Jedwali na. 4. Kiasi cha maziwa na chakula maalumu kwa
ndama……………………………………………………………
Jedwali na.5. Umri
na uzito unaoshauriwa kupandisha mtamba…………………………………………………........................32
SHUKRANI
Shukrani za pekee zinatolewa kwa walioshiriki kikamilifu katika urahisishaji
wa uandaaji wa kitabu hiki kijitabu hiki hasa FARM Africa.
Shirika la Isangati Agricultural
Development Organiztion (IADO) pia linatoa shukrani za pekee kwa kwa wadau wengine ambao utafiti wao kwa namna
moja au nyingine umefanikisha kuandaliwa Kwa kitabu hiki.
UFUGAJI WA
NG’OMBE.
A.UFUGAJI BORA WA
NG’OMBE WA ASILI
1.0 .UTANGULIZI:
Ng’ombe
ni mnyama jamii ya nyati ambaye hufugwa na mwanadamu. Nchini Tanzania ng’ombe
ni mnyama mkubwa kuliko wanyama wengine wote wanaofugwa vijijini. Ng’ombe
huwapatia wanadamu nyama, maziwa, ngozi na mbolea. Ng’ombe hufugwa katika mikoa yote ya Tanzania.
Ufugaji
holela wa ng’ombe ni ule usiozingatia kanuni na misingi ya ufugaji na una
madhara makubwa. Madhara hayo ni pamoja na:
Ø Kupata
mapato duni
Ø Uharibifu wa mazingira
Ø Ugonvi na migogoro katika jamii.
Ø Kutumia muda mwingi katika kuchunga badala ya shughuli nyingine
Ø Ni rahisi ng’ombe kushambuliwa na kueneza magonjwa
Ø Watoto hukosa elimu kwa kuwa hujihusisha na kuchunga ng’ombe
Ø Malisho duni kutokana na kufunga ng’ombe kuliko uwezo wa nyanda
husika
Ø Ufugaji huu hauzingatii ubora bali wingi wa mifugo.
2.0. AINA
ZA NG’OMBE WALIOPO NCHINI TANZANIA.
2.1.Ng’ombe
wa asili
i.
Zebu
ii.
Ankole
iii.
Boran
2.2.
Ng’ombe wa Kigeni/Kisasa
i.
Friesian
ii.
Ayrshire
iii.
Guensey
iv.
Jersey
v.
Brown Swiss
vi.
Sahiwal
2.3.Ng’ombe
Chotara
Ng’ombe
chotara ni wale waliopatikana kutokana na kuchanganya damu za aina mbili au
zaidi za ng’ombe wa kigeni na wa asili. Ng’ombe chotara wana sifa bora
mchanganyiko za ng’ombe wa kigeni na asili. Mpwapwa;
wamezalishwa kutokana na ng’ombe aina ya Boran, zebu, sahiwal na ng’ombe kutoka
Ulaya.
3.0. SIFA
ZA NG’OMBE WA ASILI.
i.
Wana uwezo wa kustahimili magonjwa
ii.
Hustahimili muda mrefu bila malisho yakutosha
iii.
Wanaweza kutembea mwendo mrefu kutafuta maji na malisho
iv.
Nyama na maziwa yao yana ladha nzuri
v.
Maziwa yao yana mafuta mengi kuliko ya ng’ombe wa kisasa
3.1.Mapungufu
ya ng’ombe wa asili
i.
Wana umbile dogo
ii.
Huchukua muda mrefu kuzaa (Ndama moja kila baada ya miaka mwili)
iii.
Hutoa maziwa kidogo
4.0. KOO
ZA NG’OMBE WA ASILI NA SIFA ZAO.
4.1.Zebu
i.
Wana nundu
ii.
Wana pembe fupi
iii.
Wana umbo dogo
iv.
Wana rangi nyingi tofauti tofauti katika sehemu mbalimabali
v.
Wanapatikana katika mikoa yote ya Tanzania
4.2.
Ankole
i.
Ng’ombe jike hawana nundu ila madume wana nundu ndogo
ii.
Wana pembe kubwa na ndefu
iii.
Hushambuliwa na magonjwa zaidi kuliko Zebu
iv.
Hutoa maziwa kidogo hivyo sio wazuri kuwafuga kwa ajili ya maziwa
v. Wanapatikana
katika mikoa ya kanda ya ziwa Victoria
4.3.
Boran
i.
Wana umbile kubwa
ii.
Wana nundu kubwa
iii.
Wana pembe fupi na wengine hawana pembe
iv.
Ni ng’ombe wa maziwa na nyama
v.
Wana kua haraka kufikia uzito wa kuchinjwa
vi.
Nyama yake huweka mafuta kiasi ni laini na yenye ladha
vii.
Wana uwezo wa kuzaa ndama kila mwaka
viii.
Huzaa ndama wenye uzito mkubwa
ix.
Wanahitaji malisho mengi
Boran
wanapatikana Kenya na Tanzania katika Ranchi za Taifa mfano Ranchi ya Manyara
na
kwa baadhi ya wafugaji binafsi.
5.0. MIFUMO
YA UFUGAJI WA NG’OMBE WA ASILI.
Kuna
mifumo mbalimbali ya ufugaji katika uzalishaji wa ng’ombe wa asili.Mifumo hiyo
ni:
i.
Ufugaji huria
ii.
Ufugaji huria uliochanganyika na kilimo
iii.
Ufugaji kwenye ranchi
iv.
Ufugaji wa kulisha vyakula vya nafaka kwa wingi
5.1.0.Ufugaji
huria
Ufugaji
huria ni mfumo wa ufugaji ambapo wafugaji huhamahama ili kutafuta malisho na
maji.
Wafugaji hawa hutegemea mifugo kwa ajili ya mahitaji yao yote.
5.1.1
Faida za ufugaji huria
i.
Ni njia ya kujihami na ukosefu wa maji na malisho hasa wakati wa ukame/kiangazi
ii.
Gharama za kuendesha mfumo huu ni ndogo
5.1.2
Hasara za mfumo wa ufugaji huria
i.
Mifugohupoteza nguvu nyingi kwa kutembea masafa marefu, na hivyo kuchukua
muda
mrefu kukua na kufikia uzito wa kuchinjwa
ii.
Ni vigumu kupatiwa huduma za kijamii kutokana na wafugaji kuhamahama.
iii.
Mfumo huu husababisha uharibifu wa mazingira endapo mifugo itakuwa mingi.
iv.
Kupungua kwa aina mbalimbali za nyasi na mimea katika nyanda za malisho.
v.
Mfumo huu umekuwa chanzo kikubwa cha migogoro kati ya jamii za wafugaji na
wakulima.
vi.
Ni rahisi kwa ng’ombe kuibiwa au kupotea.
vii.
Ni rahisi mifugo kushambuliwa na wanyama wakali.
5.2.0.
Mfumo huria uliochanganyia na kilimo
Huu
mfumo wa kukuza ng’ombe wa nyama hapa Tanzania ambapo wafugaji pia ni
wakulima
wa mazao hasa ya chakula. Ng’ombe huchungwa kwenye maeneo maalumu
yaliyotengwa
mbali na mashamba ya mazao. Aidha baada ya kuvuna ng’ombe huchungwa
kwenye
mashamba.
5.2.1.
Faida za mfumo huria uliochanganyia na kilimo
i.
Mfugaji huweza kuuza mifugo na kujipatia fedh za chakula iwapo mavuno ya
mazao
yatakuwa pungufu.
ii.
Samadi huweza kuboresha mbuga za malisho na mashamba.
iii.
Mifugo pia huweza kufaidika na masalia ya mazao shambani baada ya mavuno.
5.2.2.
Hasara za mfumo huria uliochanganyia na kilimo
i.
Ni chanzo cha uharibifu wa mazingira
ii.
Ni chanzo cha kuenea kwa magonjwa
iii.
Ni chanzo cha migogoro kati ya wakulima na wafugaji
6.0. UBORESHAJI
WA NG’OMBE WA ASILI.
Ng’ombe
bora wa nyama na maziwa wanaweza kupatikana kutokana na kuchagua
ng’ombe
wenye sifa nzuri kutoka katika kundi alilonalo mfugaji na kuwaruhusu wazaliane
ili
kuendeleza kizazi.Uboreshaji huu wa ng’ombe wa asili unaweza kufanyika kwa
kupandisha
majike ya asili.Mfano Zebu na madume ya asili kama Borani au madume ya
kisasa.
6.1.0.
Uchaguzi wa ng’ombe bora
Mfugaji
anashauriwa achague na aruhusu ng’ombe wenye sifa zifuatazo kuzaliana ili
hatimaye
awe na kundi la wanyama walio bora.
i.
Madume yenye maumbile makubwa yenye uwezo wa kupanda majike
ii.
Majike yanayozaa ndama mwenye uzito mkubwa kila mwaka.
iii.
Majike yenye kutoa maziwa mengi
iv.
Majike yasiyopata matatizo wakati wa kuzaa.
6.1.1.
Uchaguzi wa majike bora
i.
Atokane na koo zenye uwezo wa kutoa maziwa ya kutosha kulisha ndama ili akue
haraka
ii.
Awe na uwezo mkubwa wa kumlea ndama
iii.
Astahimili magonjwa na kumudu hali ya mazingira anakofugwa
iv.
Awe na uwezo wa kuzaa kila mwaka
6.1.2.
Uchaguzi wa dume bora
i.
Anayekuwa haraka
ii.
Awe na uwezo wa kustahimili magonjwa na hali ya mazingira ya eneo la kufuga
iii.
Awe na umbo halisi la dume bora
iv.
Shingo kubwa
v.
Kifua kipana
vi.
Awe na miguu imara isiyokuwa na matatizo.
vii.
Awe na uwezo wa kutambua majike yaliyo kwenye joto,kuyapanda kwa wakati
muafaka
na kuweka mimba
viii.
Awe na utulivu lakini siyo mwenye aibu na mgomvi
ix.
Awe na mapumbu yanayolingana
x.
Asiwe mgonjwa kama vile magonjwa ya zinaa ili kuepuka maambukizi kwa majike.
Angalizo:
Chagua
dume asiye na mahusiano ya karibu na majike ili kupunguza kutokea kwa vilema
na
magonjwa ya kurithi.
7.0. UZALISHAJI
WA NG’OMBE WA ASILI.
Ng’ombe
chotara ni wale waliopatikana kutokana na kuzalisha aina mbili au zaidi za
ng’ombe
wa kigeni na wa asili. Ng’ombe chotara wana sifa bora mchanganyiko za
ng’ombe
wa kigeni na wa asili.
7.1.1.
Upandishaji
Ni
tendo la ng’ombe dume kumpanda ng’ombe jike aliye kwenye joto. Madume na
majike
huwekwa pamoja katika uwiano unaoshauriwa katika kipindi chote cha mwaka na
kwa
mtindo huu ndama huzaliwa katika kipindi chote cha mwaka. Upandishaji huu ndio
unaotumika
zaidi na wafugaji wa ng’ombe wa asili.
Angalizo:
Hakikisha
unapandisha ngo’ombe ili kuwezesha ndama wengine kuzaliwa wakati kuna
malisho
na maji ya kutosha.
7.1.2.
Kupandisha kwa wakati/muda maalum
Upandishaji
kwa wakati maalumu hutumika pale inapotakiwa ng’ombe wengi wapate
mimba
na kuzaa kwa wakati mmoja ambapo kuna maji na malisho ya kutosha. Madume
kwa
kawaida huchanganywa na majike kwa wakati uliopangwa.
7.1.3.
Faida zake.
i.
Kurahisisha utunzaji wa ndama kwa kuwa na ndama wengi kuzaliwa kwa wakati
mmoja
badala ya ndama mmoja mmoja au wachache kila wakati.
ii.
Kulenga soko la mifugo kwa kuzalisha ndama wengi watakao kuwa tayari kuuzwa
kwa
wakati mmoja.
iii.
Kuoanisha upatikanaji wa malisho mengi na bora zaidi na kuzaliwa kwa ndama
ngo’ombe
wakipanda malisho bora na ya kutosha watatoa maziwa kwa wingi,
ndama
watakuwa haraka na mazao yanayokusudiwa yanapatikana mapema
iv.
Inasaidia kuwatambua ng’ombe kwenye kundi ambao hawapati mimba
Angalizo:
Umakini
unahitajika katika kumwondoa ng’ombe ambaye hajapandwa kwa wakati huo.
8.0. UBORESHAJI
NA USIMAMIZI WA MALISHO YA ASILI.
Chakula
kikuu cha ng’ombeni nyasi na majani jamii ya mikunde ambayo haia madhara kwa
afya
ya mnyama.
8.1.0.
Malisho ya Asili.
Malisho
haya kwa kawaida hukua haraka na kupoteza viinilishe muhimu, kwa muda mfupi
baada
ya mvua. Malisho ya asili huwa na viinilishe vinavyotosheleza mahitaji ya
mifugo na
wakati
wa kiangazi malisho huwa duni na yasiyotosheleza. Wakati malisho yanatosheleza
ng’ombe
huwa na uzito wa kuridhisha tofauti na wakati wa kiangazi ambapo ng’ombe
hupungua
uzito. Malisho ya asili ya jamii ya nyasi huwa na upungufu wa viinilishe
hususani
protini.
Mikunde ina tabia yakutopungua viinilishe haraka ikilinganishwa na nyasi.
8.1.1.
Malisho yaliyoboreshwa
Malisho
ya asili yanaweza kuboreshwa kwa kuongeza mimea aina ya mikunde, kuongeza
nyasi
bora kwenye malisho, kuongeza samadi kwenye mbuga za malisho. Malisho
yaliyoboreshwa
yana uwezo wa kuwafanya wanyama wakue haraka na kufikia uzito wa
kuchinjwa
mapema.
8.1.2.
Taratibu za kuboresha malisho/ Mambo ya kuzingatia
i.
Uwezo wa kuvumilia hali ya hewa na mazingira yaliyopo
ii.
Yawe yenye kuvumilia magonjwa na wadudu waharibifu
iii.
Yawe yasiyozidiwa nguvu na magugu
iv.
Yawe yenye kustahimili kuchungwa
Inafaa
maeneo ya kuchungia/kulishia yatengwe na kugawanywa katika sehemu ambazo
nyasi
zitaoteshwa na kukuzwa. Hatimaye nyasi hizo zichungwe kwa nyakati tofauti ili
kuepuka
uharibifu na kuhakikisha kuwa nyasi zinatosheleza vipindi vyote vya mwaka.
Utaratibu
huo utasaidia pia kupunguza uwezekano wa mifugo kuambukiza magonjwa.
8.1.3.
Uhifadhi wa malisho
Malisho
hupatikana kwa wingi wakati wa masika, na wakati huo yana ubora unaotakiwa.
Wakati
wa masika, mifugo hula malisho na kusaza ambapo wakati wa kiangazi malisho
huwa
haba na virutubisho hupungua ili kuwa na uhakika na upatikanaji na chakula cha
kutosha
na bora wakati wote, ni muhimu kuhifadhi malisho ya ziada katika kipindi hicho.
8.1.4.
Njia za kuhifadhi malisho.
Kuna
njia kuu mbili za kuhifadhi malisho nazo ni;
i.
Kuyakausha (Hei)
ii.
Kuyavundika (Saileji)
8.1.5.
Kuyakausha (Hei).
Hei
ni majani makavu ambayo yanaweza kulishwa wanyama yangali shambani au kuvunwa
na
kufungwa kwenye marobota kisha kuhifadhiwa kwa matumizi ya baadaye.
8.1.6.
Hatua ya kutayarisha
i.
Vuna majani yanapoanza kutoa maua
ii.
Yaanike na yageuze majani mara moj au mara mbili kwa siku ili yakauke vizuri
iii.
Ukaushaji huchukua siku tatu hadi sita kutegemea aina ya majani au hali ya hewa
iv.
Majani yakiisha kauka yafunge kwenye marobota
v.
Yahifadhi marobota sehemu isiyoingiza mvua au unyevu
vi.
Marobota ya majani makavu yanaweza kutengenezwa kwa mashine au kwa
kutumia
makasha ya mbao.
vii.
Mfugaji mdogo anashauriwa kutumia makasha ya mbao kwa kutengeneza
marobota
hayo.
viii.
Makasha ya mbao yanaweza kutengenezwa kwa kutumia vipimo vifuatavyo,urefu
sentimita 75, upana sentimita 45 na kina sentimita 35.
ix.
Majani yaliyofungwa katika marobota hutumia sehemu ndogo ya kuhifadhia na pia
hupunguza
upotevu.
x.
Mfugaji anaweza kukadiria kiasi cha malisho atakayotumia kulisha ng’ombe wake
kwa
msimu wa kiangazi.
8.1.7.
Masalia ya mazao shambani
Masalia
ya mazao kutoka shambani yanaweza kutumiwa ili kufidia chakula ambacho
ng’ombe
amekikosa kutokana na uhaba wa majani wakati wa kiangazi. Masalia yanaweza
kuwa
ya mabua ya nafaka mbalimbali kama vile mahindi, mtama, mpunga, ulezi, ngano au
uwele.
Mengine ni majani ya viazi vitamu, miwa au majani ya jamii ya mikunde kama vile
maharage,kunde,
njugu mawe au mbaazi.
Masalia
yanaweza kutumiwa na ng’ombe moja kwa moja bila kuboreshwa. Hata hivyo
ng’ombe
hawezi kula kwa wingi na hivyo inashauriwa kuyanyunyuzia molasses au magadi
ili
ng’ombe aweze kula mengi zaidi.
8.1.8 .Maji
Maji
ni muhimu katika kupoza joto la mwili kutengeneza maziwa, kusafirisha
virutubisho
na
kutoa uchafu mwilini kwa njia ya mkojo,kinyesi kupumua na jasho. Ng’ombe
akipata
maji
ya kutosha hukua vizuri, huwa mwenye afya na hutoa maziwa mengi na bora. Kiasi
cha
asilimia 85 hadi 87 ya maziwa ni maji. Ng’ombe anapokosa maji hukosa hamu ya
kula
na
hali hiyo ikiendelea hupungukiwa maji na hupoteza uzito. Ng’ombe anaweza kupata
maji
kwa njia zifuatazo;
i.
Kunywa
ii.
Kula vyakula vyenye maji maji
8.1.9.
Vyakula vya ziada
Hakikisha
mifugo yako wanapata vyakula vya ziada kama vile
i.
Pumba za mahindi, mtama,ngano
ii.
Mashudu ya pamba au alizeti
iii.
Madini
iv.
Vitamini
9.0 SHUGHULI
ZA UTUNZAJI BORA WA AFYA YA MIFUGO.
9.1.
Uogeshaji.
Mifugo
waogeshwe mara kwa mara ili kuepukana na magonjwa yaenezwayo na kupe
pamoja
na ndorobo. Uogeshaji unaweza kufanyika kwa kutumia pampu za mgongoni
(knapsack
sprayers) au kuwatumbukiza katika josho lililotiwa dawa ya kuogeshea.
9.2.
Kuwapa dawa ya minyoo
Mifugo
wapatiwe dawa za minyoo mara kwa mara ili kuhakikisha ukuwaji wao na utoaji
wa
maziwa uendelee vizuri. Mifugo wapewe dawa za minyoo kila baada ya miezi mitatu
9.3.
Kuhasi
Ndama
dume wasiohitajika kwa ajili ya kuzalisha baadaye wahasiwe kwa njia ya
operesheni
au kwa kutumia koleo au badizo iwapo ndama ni wakubwa.
9.4. Kuwapa
ndama alama za utambulisho
Ndama
wapewe namba au alama za utambulisho mara wafikiapo miezi 6 tangu kuzaliwa.
Utambulisho
unaweza kuwa wa chuma au plastiki chenye nambari kwenye sikio,mikato
maalumu
katika masikio au chapa katika sehemu malum za mwili.
9.5.
Kuondoa vichomozo vya pembe
Ndama
waondolewe pembe katika mwezi wa kwanza tangu kuzaliwa. Tumia chuma cha
moto
kuchoma kichomozo chote cha pembe.
10.0.
MAZAO YATOKANAYO NA MIFUGO.
Kutokana
na ufugaji wa ng’ombe wa asili, tunapata mazao yafuatayo:
i. Nyama
ii.
Maziwa
iii.
Mbolea
iv.
Ngozi
v.
Kwato
vi.
Mifupa
vii.
Damu
viii.
Pembe
10.1.
Maziwa
Maziwa
yanaweza kusindikwa na kupata mazao mengine ya mifugo kama vile samli, siagi
na
jibini
10.2.
Pembe na kwato
Mazao
haya vile vile yanaweza kutumika kutengeneza gundi, vifungo, mapambo na pia
vyombo
vya kunywea vinywaji mbalimbali na pia kama tarumbeta.
10.3.
Ngozi
Ni
zao linaloweza kutumika katika kutengenezea mikanda, viatu na mikoba ya ngozi.
10.4.
Damu na Mifupa
Damu
na mifupa huweza kutumika kutengenezea vyakula vya kuku na mifugo mingine.
Matumizi
mengine ya Ng’ombe wa asili:
i.
Wanyama kazi
ii.
Kutolea mahali
iii.
Kipimo cha utajiri
iv.
Ajira
v.
Kuongeza kipato
vi.
Kinga dhidi ya majanga
vii.
Kufanyia matambiko
11.0. UTAMBUZI
WA MWANZO WA MAGONJWA YA MIFUGO.
11.1 .Sifa
za mnyama mwenye afya
i.
Mchangamfu wakati wote macho maang’avu huku mkia na masikio vikimsaidia
kufukuza
inzi
ii.
Kula na kucheua, kunywa maji vizuri kila siku
iii.
Kuonyesha ushirikiano na kutembea pamoja kwenye kundi
iv. Kutembea
vizuri
v.
Anastuka na kukimbia anapostuliwa na mnyama hatari anapomkaribia kama vile
mbwa
mwitu, fisi, chui, simba.
vi.
Mwili wake una uwezo mkubwa wa kukibadili chakula anachokula kutoa mazao ya
kutosha
kama vile maziwa.
vii.
Anaonekana mwenye nguvu na kwa wale wanaoendelea kukuna wanaongezeka
uzito
kwa muda mfupi
viii.
Kwa mnyama anayekamuliwa mara kwa mara kupiga kelele za kumtafuta mtoto
wake,kiwele
huwa kimejaa maziwa, chuchu huwa wakati mwingine zimetanuka
upande
kwa ajili ya kujaa maziwa
ix.
Ngozi ya mnyama husisimka mara kwa mara wadudu wapomtambaa
x.
Kwa madume, huwa wana hamu ya kuwapanda majike wanaoingia kwenye joto.
Miili
yao hujengeka vizuri. Pumbu hujengeka na kukaa vizuri kwenye nafasi yake
(yaani
katikati ya miguu)
xi.
Pua na midomo huwa na unyevu unyevu wakati wote.
xii.
Ngozi kuwa na ulaini unaotakiwa na manyoya hung’aa.
xiii.
Kwa kawaida unapo mkaribia mnyama endapo amekaa chini ni lazima atanyanyuka
11.2.
Dalili za Mnyama anayeumwa
i.
Hukosa hamu ya kula na kunywa maji
ii.
Mwili kunyong’onyea na kuonekana mchovu
iii.
Mnyama kutembea pole pole na kwa taabu na mara nyingi hujitega na wenzake
iv.
Pua zake na midomo huonekana kukauka.
v.
Kupunguka kwa kiwango cha uzalishaji kama vile maziwa. Kwa madume huduwaa
na
kuinamisha shingo chini na kukosa hamu ya kuwapanda majike wanaoingia
kwenye
joto.
11.3.
Vyanzo vya magonjwa
Magonjwa
mengi ya mifugo husambazwa na vijidudu ambao huingia kwenye mfumo wa
damu
na kusababisha homa na baadae madhara makubwa. Mangonjwa mengi ya mifugo
husababishwa
na vyanzo kutoka nje ya mwili wa mnyama mfano mazingira machafu
anayoishi
mnyama, vitu vinavyopelekea vidonda (Vitu vyenye ncha kali) husababisha
vidonda
ambapo vimelea vinaweza kukaa.Pia mnyama anaweza kupata ugonjwa kutokana
na
hali za ndani ya mwili kama upungufu wa lishe, mfano: madini, na na magonjwa ya
kulithi.
Mfano
wa wadudu hao ni;
11.4.
Vimelea (bacteria)
Mfano
wa magonjwa yanayosababishwa na bacteria ni chambavu, Blackquarter, Kimeta,
Kifua
kikuuu, brucellosis (ugonjwa wa kutupa mimba) na ugonjwa wa kiwele.Ng’ombe
dume
huvimba mapumbu.
11.5 .Virusi
(virus) Otatis
Mfano
wa magonjwa yanayosababishwa na virusi ni kichaa cha mbwa (Rabies), Ugonjwa
wa
midomo,miguu (foot and mouth disease) na Sotoka (Rinderpest)
11.6.
Protozoa
Magonjwa
yanayo sababishwa na protozoa ni kama ndigana baridi, ndigana kali, ndigana
mkojo
damu, ndigana maji moyo na nagana.
Angalizo:
Magonjwa
yote ya Ndigana husambazwa na makupe, wakati ugonjwa wa nagana
husambazwa
na ndorobo.
11.7.
Lishe duni.
Upungufu
wa viinilishe katika chakula cha mifugo husababisha madhara katika mwili kama
ifuatavyo;
i.
Husababisha majike kutopata joto mapema
ii.
Ndama kuzaliwa na viungo visivyo komaa
iii.
Upungufu wa uzalishaji maziwa
iv.
Kiwango cha uzalishaji kushuka
11.8.
Vidonda/michubuko
Kupitia
vidonda au michubuko, wadudu wasababishao magomjwa huweza kuingia mwilini
kwa
mnyama
11.9.
Magonjwa ya kurithi
Kama
mmoja wa wazazi ana ugonjwa wa kurithi basi kuna uwezekano mkubwa kwa
mmoja
wa ndama watakaozaliwa kurithi ugonjwa huo
12.0. MAGONJWA
YANAYOENEZWA NA KUPE.
12.0.
Ndigana kali
12.1.1.
Dalili zake
i.
Homa kali hadi nyuzi joto 42c
ii.
Povu kutoka mdomoni na puani
iii.
Kuhara choo kilichochanganyikana na kamasi na damu
iv.
Tezi kuvimba sana na zenye joto
v.
Kuacha kula
vi.
Ukungu kwenye macho
vii.
Kifo baada ya wiki moja hadi mbili
12.1.2.
Tiba.
Butalex,
Parvexon, tiba iambatane na sindano moja ya kuondoa uvimbe kwenye mapafu
kama
hali hiyo tayari imeshajitokeza. Tumia Multivitamin ili kuongeza hamu ya kula
na
Raxis
ili kuondoa maji kwenye mapafu.
12.1.3.
Kinga/zuia.
Zingatia
uogeshaji sahihi na Chanjo ya ECF
12.2.0.
Ndigana baridi (Anaplasmosis)
12.2.1.
Dalili zake
i.
Homa hadi nyuzi joto 42C
ii.
Kukosa hamu ya chakula
iii.
Choo kigumu na makamasi na harufu mbaya
iv.
Kifo baada ya siku 8 hadi 10
12.2.2.
Tiba.
i.
Antibiotic kama vile Oxytetracycline
ii.
Imizol.
12.2.3.
Kinga.
Zingatia
uogeshaji sahihi
12.3.0
Ndigana mkojo damu (Babesiosis) ugonjwa wa kukojoa damu
12.3.1
Dalili zake
i.
Mkojo kuwa na rangi ya damu isiyokolea zambarau
ii.
Mkojo hutoka kidogo kidogo na kwa muda mrefu
iii.
Homa hadi nyuzi joto 40C
iv.
Kuacha kula
v.
Choo kigumu au kuhara wakati mwingine
vi.
Kifo baada ya wiki 1
12.3.2.
Tiba.
Berenil
ikisaidiwa na antibiotics za sindano kama vile oxytetracycline (OTC) pia tumia
Multivitamin
kuongeza hamu ya kula.
12.3.3.
Kinga
Zingatia
uogeshaji sahihi
12.4.0.
Ndigana maji moyo (heart water)
12.4.1.
Dalili zake
i.
Kizunguzungu na kuanguka,
ii.
Kifo baada ya siku 2
12.4.2.Tiba
Antibiotics
za sindano kama vile oxytetracycline. Kumbuka tiba lazima ifanywe mapema
iwezekanavyo
12.4.3.
Kinga/kuzuia.
Zingatia
uogeshaji sahihi
13.0. UTUNZAJI
WA KUMBUKUMBU.
Uwekaji
wa kumbukumbu ni muhimu sana kwa kila mfugaji. Kumbukumbu zinasaidia
katika
kujua mambo mengi kama matukio ya magonjwa, tiba, chanjona uogeshaji,
gharama
za uendeshaji kama gharama za madawa ya tiba, chanjo na uogeshaji, mishahara
ya
wafanyakazi, faida au hasara baada ya mauzo. Kumbukumbu hizi humsaidia mfugaji
Kufanya
maamuzi katika uendelezaji wa Shamba Lake.
13.1.0.
Aina za kumbukumbu
Kumbukumbu
muhimu katika ufugaji wa ng’ombe ni pamoja na idadi ya ndama
wanaozaliwa,
idadi ya ng’ombe,afya ya ng’ombe,kumbukumbu ya mapato na matumizi.
Hata
hivyo mfugaji anaweza kuongeza kumbukumbu nyingine kulingana na mahitaji na
shughuli
zake.
B.UFUGAJI BORA WA
NG’OMBE WA KISASA.
14.0.NG’OMBE WA NYAMA.
Ng’ombe wanaofaa kufugwa kwa ajili
ya uzalishaji nyama ni wale wanaokua kwa haraka na kuweka misuli mikubwa
iliyojengeka vizuri. Baadhi ya koo zenye sifa hizo ni pamoja na
Boran, Mpwapwa (nyama na maziwa), Charolais, Aberdeen Angus, pamoja na chotara
wao. Hata hivyo, nchini Tanzania ng’ombe aina ya Zebu (mfano
Ufipa,Gofo, Masai, Sukuma, Tarime, Iringa red), Sanga (Ankole) na chotara wao
ndio hutumika kama ng’ombe.
14.1.0.
Utunzaji wa ng’ombe wa nyama
Ng’ombe wengi wanaofugwa hapa nchini
Tanzania ni wa asili ambao kwa kiwango kikubwa hutumika kwa ajili ya uzalishaji
wa nyama. Hata hivyo uzalishaji wake wa nyama ni mdogo kutokana na
kasi ndogo ya kukua na kuwa na uzito mdogo wakati wanapopevuka. Hali
hii husababishwa na matunzo duni, kwa kuwa huchungwa/hulishwa kwa kutegemea
malisho peke yake ambayo hayawezi kukidhi mahitaji ya viinilishe
vinavyohitajika kwa ng’ombe.
14.1.1. Utunzaji wa
ndama
Ili kuongeza kasi ya ukuaji na
kuongeza uzalishaji wa nyama, mfugaji anapaswa kufanya mambo yafuatayo:-
v Wajengewe banda/boma imara safi na
lisilo na unyevunyevu ili kuepukana na magonjwa kama kichomi na kuhara
v Waruhusiwe kunyonya kwa muda
usiopungua miezi sita, pia wapatiwe majani laini kuanzia wanapofikia umri wa
wiki mbili ili waanze kula mapema.
v Wapatiwe maji safi na yakutosha
v Ndama dume ambao hawatahitajika kwa
ajili ya kuendeleza kizazi wahasiwe wakiwa na umri wa wiki mbili ili waanze
kula mapema.
v Wapatiwe maji safi na yakutosha
v Ndama dume ambao hawatahitajika kwa
ajili ya kuendeleza kizazi wahasiwe wakiwa na umri usiozidi miezi 3 ili wakue
haraka na kuwa na nyama nzuri.
v Wawekwe alama au namba za
utambulisho kati ya siku ya kwanza na ya tano kwa ndama wote, mfano kuvalishwa
hereni kwenye masikio, kwa ajili ya urahisi wa udhibiti wa umiliki na utunzaji
kumbukumbu.
v Ndama wachungwe eneo tofauti na
ng’ombe wakubwa kuepuka maambukizi ya minyoo na magonjwa na
14.1.2.Utunzaji wa ndama
baada ya kuachishwa kunyonya hadi kupevuka (miezi 6 – 24).
Ndama wa umri huu anatakiwa apatiwe:
1) Malisho bora na maji safi ya kutosha
wakati wote
2) Vyakula vya ziada ili kukidhi
mahitaji ya mwili (mifano ya vyakula mchanganyiko imeonyeshwa kwenye jedwali
Na. 3 ) na
3) Tiba na kinga dhidi ya magonjwa
hususan kinga ya kutupa mimba (S19) kwa ndama jike watakaotumika kuendeleza
kundi.
4) Katika kipindi cha miezi 6 hadi 24
mfugaji anashauriwa kuchagua ndama watakaoingizwa katika kundi la wazazi na
wanaobaki wawe katika kunenepesha kwa ajili ya nyama.
14.1.3.Unenepeshaji wa
ng’ombe wakubwa.
Ng’ombe kwa ajili ya nyama anaweza
kuchinjwa akiwa na umri wa kuanzia miezi 3 kulingana na mahitaji ya
soko. Kwa kawaida hapa Tanzania ng’ombe huchinjwa wakiwa na umri wa
kuanzia miezi 18 kwa ng’ombe wa kigeni na zaidi ya miezi 36 kwa ng’ombe wa
kigeni na zaidi ya miezi 36 kwa ng’ombe wa asili.
14.1.4.Mkulima atapata faida kwa
kuzingatia yafuatayo.
Ili mfugaji aweze kupata faida kutokana na ufugaji wa
ng’ombe wa nyama anapaswa afanye yafuatayo:-
1) Afuge aina ya ng’ombe wanaokua na
kukomaa haraka
2) Anenepeshe ng’ombe kwa muda wa miezi
3 – 6 kabla ya kuchinjwa. Unenepeshaji huongeza ubora wa nyama na
kipato kwa mfugaji.
3) Awapatie chakula chenye mchanganyiko
wenye viinilishe vya kutosha viinilishe vya kutia nguvu na joto mwilini viwe na
uwiano mkubwa kuliko vingine (Jedwali Na.3), na
4) Auze ng’ombe mara wanapofikisha umri
na uzito unaohitajika katika soko ili kuepuka gharama za ziada.
Jedwali na.1. Mfano
wa mchanganyiko wa chakula kwa ajili ya unenepeshaji.
AINA
YA CHAKULA
|
KIASI
KWA KILO
|
Majani
makavu ya mpunga/NganoHey
|
23.3
|
Molasis
|
44.72
|
Mahindi
yaliyorazwa
|
18.94
|
Mashudu
ya Alizeti/pamba
|
11.4
|
Madini
mchanganyiko
|
0.7
|
Chumvi
|
0.47
|
Urea
|
0.47
|
Jumla
|
100
|
14.2.0. Malisho bora na
vyakula vya ziada.
14.2.1.Uzalishaji na
uhifadhi wa malisho bora na vyakula vya ziada.
Chakula kikuu cha ng’ombe ni nyasi,
vyakula vingine ni pamoja na miti malisho, mikunde na mabaki ya
mazao. Ili kupata malisho misimu yote ya mwaka ni muhimu kuvuna na
kuhifadhi malisho kipindi yanapopatikana kwa wingi. Inawezekana
kupanda malisho mengi kuliko kiasi kinachohitajika msimu mmoja/wakati wa mvua,
kuyavuna yanapofikia hatua ya kutoa maua na kuyahifadhi (mfano wa malisho
yanayoweza kupandwa ni mabingobingo, Guatemala, African fox-tail, desmodium,
centrosema, lukina n.k). Malisho yakupandwa ni vizuri yawe na
mchanganyiko wa jamii ya nyasi, mikunde na miti malisho.
14.2.2.Masalia ya mazao
shambani.
Masalia ya mazao shambani kama vile
mabua, magunzi, majani ya mikunde, viazi, ndizi, mpunga, na mengineyo yanaweza
kukusanywa na kuhifadhiwa vizuri kama chakula cha ng’ombe.
14.2.3.Malisho ya miti
na matunda yake.
Malisho yatokanayo na miti ya
malisho na matunda yake yanaweza kutumika kama malisho ya
ng’ombe. Majani na matunda ya miti ya lukina, sesibania, migunga na
mbaazi yanaweza kukaushwa na kuhifadhiwa kwa ajili ya kulisha ng’ombe.
14.2.4.Vyakula vya ziada
Ili kukidhi mahitaji ya viinilishwe
kulingana na kiwango cha uzalishaji, ng’ombe anatakiwa kupewa vyakula vya
ziada. Vyakula hivyo vinatokana na mchanganyiko wa vyakula
mbalimbali. Michanganyiko hii inategemeana na upatikanaji
wa malighafi katika maeneo husika.
Mifano ya mchanganyiko huo ni kama ifuatavyo:-
Jedwali na.2 Mfano wa kwanza wa chakula cha ziada
AINA
YA CHAKULA
|
KIASI
(KILO)
|
Pumba
za mahindi
|
47
|
Mahindi
yaliyoparazwa
|
20
|
Mashudu
ya alizeti/pamba
|
20
|
Unga
wa lukina
|
10
|
Chokaa
ya mifugo
|
2
|
Chumvi
|
1
|
Jumla
|
100
|
Mfano wa pili wa chakula cha ziada
ni tofali la kulamba lenye urea ambalo mchanganyiko wake ni:-
Jedwali
na. 3. Mfano wa kwanza wa chakula cha ziada
NGOMBE
|
WALIOACHA
KUNYONYA.(KG)
|
WA MAZIWA (KG)
|
|
1
|
Pumba
za mahindi
|
66
|
56
|
2
|
Pumba
laini za mpunga
|
-
|
10
|
3
|
Mashudu
ya alizeti(meusi)
|
25
|
25
|
4
|
Chokaa
|
3
|
3
|
5
|
Mifupa
iliyochomwa na kusagwa
|
3.5
|
3.5
|
6
|
Chumvi
|
1
|
1
|
7
|
Madini
yenye colt+salfa
|
1.5
|
1.5
|
|
JUMLA
|
100
|
100
|
14.2.4.Mambo mhimu ya kuzingatia.
Mfugaji anatakiwa kuzingatia
yafuatayo ili kupata tija katika ufugaji:-
v kulisha mchanganyiko wa nyasi,
mikunde na mchanganyiko wa madini na vitamin
v kutenga maeneo kwa ajili ya kulisha
ng’ombe kwa mzunguko pamoja na kupanda malisho katika mfumo huria na nusu huria
na
v kuvuna nyasi na mikunde inapofikia
hatua ya kutoa maua na kuyahifadhi kwa matumizi wakati wa uhaba wa malisho
hususan wakati wa kiangazi.
14.2.4.0.Njia za kuhifadhi malisho
Malisho yanaweza kuhifadhiwa kwa
kuyakausha (Hei) au kuyavundika (Sileji).
14.2.4.1.Hei
Hei ni majani yaliyohifadhiwa kwa
kukaushwa baada ya kukatwa au kuachwa kukauka yakiwa shambani kwa matumizi ya
baadaye.
Katika kutengeneza hei yafuatayo yazingatiwe:-
1) Vuana malisho
yanapoanza kutoa maua
2) Yaanikwe kwa siku 3 hadi 6 kutegemea
aina ya malisho na hali ya hewa na yageuze mara 1 au 2 kwa siku ili yakauke
vizuri.
3) Yafungwe katika marobota baada ya
kukauka inawezekana kutumia kasha la mbao lenye vipimo
vifuatavyo:- Urefu sentimeta 75, upana sentimeta 45 na kina
sentimeta 35 au mashine na zana za kufunga marobota ya hei na
4) Hifadhi marobota juu ya kichanja ili
kuzuia maji yasiingie unyevu na kuharibiwa na wadudu.
14.2.4.2.Sileji.
Sileji ni majani yaliyokatwakatwa na
kuvundikwa. Madhumuni ya kuyavundika ni kuyawezesha kubaki na ubora
wake hadi wakati yatakapotumika katika kutengeneza sileji yafuatayo
yazingatiwe:-
v Tengeneza sileji kwa kutumia majani
yenye sukari nyingi kama mahindi au mabingobingo na mikunde, mabaki ya
viwandani kama molasis,
v Andaa shimo au mfuko wa plastiki
kulingana na kiasi cha majani yaliyovunwa.
v Vuna majani ya kuvundika katika umri
wa kuanza kutoa maua. Endapo majani yaliyovunwa ni teketeke yaachwe
kwa siku moja yanyauke kupunguza kiwango cha maji.
v Katakata majani uliyovuna katika
vipande vidogovidogo,
v Tandaza majani uliyokatakata ndani
ya shimo au mfuko katika tabaka nyembamba na kushindilia ili kuondoa hewa yote.
v Funika shimo ulilojaza majani kwa
plastiki ikifuatiwa na udongo.
v Sileji itakuwa tayari kutumika
kuanzia siku 21 na
v Sileji iliyofunguliwa kwa ajili ya
matumizi ifunikwe haraka iwezekanavyo ili kuzuia kuharibika.
v Sileji inaweza kubaki na ubora
katika shimo kwa muda mrefu kama haitafunguliwa na kuachwa wazi kwa muda mrefu.
15.0. NG’OMBE WA MAZIWA.
15.1.0.Sifa za ng’ombe wa maziwa
zifuatazo:-
Ø Umbo lililopanuka kwa nyuma na
kupungua kuelekea kichwani.
Ø Mgongo ulionyooka kuanzia mabegani
kuelekea mkiani
Ø Miguu ya nyuma mirefu iliyonyooka,
minene yenye kuacha nafasi kwa ajili ya kiwele na kwato imara.
Ø Kiwele kiwe kikubwa chenye chuchu
nne, ndefu na unene wa wastani
Ø Nafasi kati ya chuchu na chuchu iwe
ya kutosha na
Ø Endapo ng’ombe anakamuliwa awe na
kiwele kikubwa kilichoshikamana vizuri mwilini, na mishipa mikubwa kwenye
kiwele iliyosambaa.
Aina ya ng’ombe wa maziwa wanaofugwa
kwa wingi nchini ni pamoja na Friesian, Ayrshire, jersey, Mpwapwa, Simmental na
chotara watokanao na mchangoayiko wa aina hizo na Zebu.
16.0.UTUNZAJI WA MAKUNDI MABALIMBALI YA NG’OMBE WA MAZIWA
KULINGANA NA UMRI NA HATUA YA UZALISHAJI
16.1.0.Utunzaji wa ndama
Mfugaji anapaswa kutunza ndama
vizuri kwa lengo la kupata ng’ombe wengi na bora kwa ajili ya
maziwa. Mambo muhimu ya kuzingatia katika utunzaji wa ndama tangu
kuzaliwa hadi kuachishwa maziwa ni pamoja na
Ø Kuhakikisha kuwa ndama anapakwa dawa
ya kuzuia maambukizi ya viini ya magonjwa kupitia kwenye kitovu, kwa mfano dawa
joto (Tincute of Iodine) mara baada ya kuzaliwa na
Ø Ndama apatiwe maziwa ya awali yaani
dang’a (colostrums) mara baada ya kuzaliwa kwa lengo la kupata kinga ya mwili
dhidi ya magonjwa. Aidha, aendelee kunyonya maziwa hayo kwa muda wa
siku 3-4.
16.1.1.Utenganezaji wa maziwa kwa
ajili ya ndama.
Endapo jike aliyezaa amekufa au
hatoi maziwa, apewe dang’a toka kwa ng’ombe mwingine kama yupo au dang’a
mbadala, ambayo inaweza kutengenezwa kwa kuchanganya vitu vifuatavyo:-
Lita moja ya maziwa yaliyokamuliwa
wakati huohuo.
Lita moja ya maji yaliyochemshwa na
kupozwa hadi kufikia joto la mwili.
Kijiko kimoja cha chai cha mafuta ya
samaki (cod liver oili).
Mafuta ya nyonyo vijiko vya chai 3
na
Yai moja bichi.
Koroga mchanganyiko huo, weka katika
chupa safi.
16.1.2.Unyweshaji wa maziwa kwa
ndama.
Ndama anyweshwe kabla
haujaopoa. Ndama anyweshwe mchanganyiko huo mara 2 kwa siku kwa muda
wa siku 3 mfululizo na kila mara mchanganyiko uwe mpya. Wakati wa
kunywesha chupa iwekwe juu ya kidogo ili asipaliwe.Endapo ndama
hawezi kunyonya ng’o mbe akamuliwe na ndama anyweshwe maziwa kwa njia ya chupa
kwa kuzingatia usafi wa maziwa na chupa.Ndama aendelee kunyweshwa maziwa kwa
kiasi kama ilivyoonyeshwa kwenye Jedwali Na. 1. Ndama aanze kuzoeshwa kula
nyasi laini, pumba kidogo na maji safi wakti wote kuanzia wiki ya 2 baada ya
kuzaliwa na ndama aachishwe kunyonya au kupewa maziwa akiwa na umri wa miezi
3. Mfugaji ahakikishe kwamba ndama anayeachishwa kunyonya ana afya
nzuri.
Jedwali na. 4. Kiasi cha maziwa na chakula maalumu kwa
ndama.
UMRI
(WIKI)
|
KIASI
CHA MAZIWA KWA SIKU (LITA)
|
KIASI
CHA CHAKULA MAALUM CHA NDAMA KWA SIKU (KILO)
|
1
|
3.0
|
0.0
|
2
|
3.5
|
0.0
|
3
|
4.0
|
0.0
|
4
|
4.5
|
0.0
|
5
|
5.0
|
0.1
|
6
|
5.0
|
0.2
|
7
|
5.0
|
0.3
|
8
|
4.0
|
0.4
|
9
|
3.0
|
0.7
|
10
|
2.0
|
1.0
|
11
|
1.5
|
1.25
|
12
- 16
|
0.75
|
1.5
|
Vyombo vinavyotumika kulishia ndama
visafishwe vizuri kwa maji yaliyochemshwa, sabuni na kukaushwa.
16.1.2.Matunzo mengine ya ndani ni pamoja na:-
a) Kuondoa pembe kati ya siku 3 hadi 14
mara zinapojitokeza ili kuzuia wanyama kuumizana na kuharibu ngozi,
b) Kukata chuchu za ziada kwa ndama
jike
c) Kuhasi ndama dume wasiozidi umri wa
miezi 3 ambao hawatahitajika kwa ajili kuendeleza kizazi ili wakue hawatajika
kwa ajili ya kuendelea kizazi ili wakue haraka na kuwa na nyama nzuri.
d) Kuweka alama au namba za utambulisho
kati ya siku ya kwanza na ya tano, mfano kuvalishwa hereni kwenye masikio kwa
ajili ya urahisi wa udhiti wa umiliki na utunzaji kumkukumbu na,
e) Kuwapatia kinga dhidi ya maabukizi
na tiba ya magonjwa wanapougua.
Kumbuka:Huduma hizi zifanyike chini ya
maelekezo ya mtaalam wa mifugo.
16.2.0.Utunzaji wa ndama baada ya kuachishwa maziwa hadi
kupevuka (miezi – 18)
v Ndama baada ya kuachishwa maziwa
apate malisho bora na chakula mchanganyiko kuanzia kilo 2 4 kwa siku kutegemea
umri wake na
v Ndama wanapofikia umri wa miezi 18
wachaguliwe wanaofaa kuendeleza kizazi, wasio na sifa nzuri waondolewe katika
kundi.
16.2.1.Utunzaji wa mtamba
Mtamba ni ng’ombe jike aliyefisha
umri wa kupandwa (wastani wa miezi 18) hadi anapozaa kwa mara ya
kwanza. Ni muhimu kutunza vizuri mtamba ili kupata kundi bora la
ng’ombe. Miezi 3 kabla ya kupandishwa mtamba apatiwe:-
v Malisho bora
v Maji ya kutosha
v Madini mchanganyiko na
v Chakula cha ziada kiasi cha kilo 2 –
3 kwa siku, ili kuchochea upevukaji na kuongeza uzito wa mwili.
16.3.0.Utunzaji wa ng’ombe wakubwa
Kundi hili linajumuisha ng’ombe
wenye mimba, wanaokamuliwa na madume. Mfugaji anapaswa kutunza vizuri
ng’ombe wake wakubwa kwa lengo la kumpatia malisho bora na maji safi ya kutosha
kila siku. Mambo muhimu ya kuzingatia katika utunzaji wa ng’ombe
wakubwa ni pamoja na:-
- Ng’ombe
apatiwe majani makavu (hei) wastani wa kilo 10 au majani mabichi kilo 40 kwa
siku kutegemeana na uzito. Iwapo malisho hayatoshi hususan wakati wa
kiangazi apewe masalia ya mazao (viwandani na mashambani) kama molasisi, mabua,
maharage, mpunga n.k
- Ng’ombe
apewe vyakula vya ziada (pumba, mashudu, madini mchanganyiko, unga wa mifupa na
chokaa) kulingana na hatua na kiwango cha uzalishaji na
- Ng’ombe
apatiwe kinga na tiba ya magonjwa kulingana na ushauri wa mtaalam wa mifugo.
17.0.UPANDISHAJI.
Mfugaji anapaswa kumpandisha ng’ombe
kwa umri na wakati muafaka ili kuepuka matatizo ya uzazi na pia kuhakikisha
anapata ndama bora na maziwa mengi.
17.1.0. Mambo muhimu ya kuzingatia katika upandishaji.
Mambo muhimu ya kuzingatia ni pamoja
na:
v Mtamba apandishwe akiwa na umri wa
miezi 17 -24 na uzito wa kilo 230 – 300 kwa ng’ombe wa kigeni na umri wa miezi
30 – 36 na uzito wa kilo 200 kwa ng’ombe wa asili. (Rejea jedwali Na
2)
v Ng’ombe aliyekwisha zaa apandishwe
siku 60 baada ya kuzaa na
v Siku 18 – 23 baada ya kupandishwa,
ng’ombe achunguzwe kama ana dalili za joto ili apandishwe
tena. Iwapo ng’ombe ataendelea kuonyesha dalili za joto baada ya
kupandishwa mara tatu mfugaji apate ushauri wa mtaalam wa mifugo.
Jedwali na.5. Umri na uzito unaoshauriwa
kupandisha mtamba
AINA
YA NG’OMBE
|
UZITO
(KG)
|
UMRI
(MIEZI)
|
Friesian
|
240
– 300
|
18
– 24
|
Ayrshire
|
230
– 300
|
17
– 24
|
Jersey
|
200-
250
|
18
– 20
|
Mpwapwa
|
200
– 250
|
18
– 20
|
Chotara
|
230
– 250
|
18
– 24
|
Boran
|
200
– 250
|
24
- 36
|
Zebu
|
200
|
30
-36
|
Ni muhimu mfugaji akazitambua dalili
za ng’ombe anayehitaji kupandwa ili aweze kumpandisha kwa
wakati. Dalili hizo ni pamoja na
Ø Kupiga kelele mara kwa mara
Ø Kutotulia/kuhangaika
Ø Kutokwa na ute mweupe usiokatika
ukeni
Ø Kupenda kupanda wenzake na husimama
akipandwa na wenzake na
Ø Kunusanusa ng’ombe wengine
Ø Ng’ombe akionyesha dalili za joto
apandishwe baada ya masaa 12, kwa kuhimilisha au kwa kutumia dume bora (kwa
mfano, akionyesha dalili asubuhi apandishwe jioni na akionyesha dalili jioni
apandishwe asubuhi).
17.3.0.Uhimilishaji.
Uhimilishaji ni njia ya kupandikiza
mbegu kwa ng’ombe jike kwa kutumia mrija. Faida za uhimilishaji ni
pamoja na kusambaza mbegu bora kwa haraka na kwa gharama nafuu, kupunguza
gharama za kutunza dume na kudhibiti magonjwa ya uzazi.
17.3.1. Mambo ya kuzingatia ili mkulima afaidike.
Ili mfugaji anufaike na huduma hii
anapaswa kufanya yafuatayo:-
Ø Kuchunguza kwa makini ng’ombe mwenye
dalili za joto
Ø Kumjulisha mtaalam wa uhimilishaji
mapema ili kuwezesha zoezi hili kufanyika kwa wakati.
Ø Kuchunguza kama ng’ombe atarudi
kwenye joto siku ya 18 – 23 baada ya kupandishwa na
Ø Ng’ombe aliyepandishwa apimwe mimba
siku 60 hadi 90 baada ya kupandishwa.
17.4.0.Matunzo ya ng’ombe mwenye mimba
Ng’ombe mwenye mimba huchukua miezi
9 hadi kuzaa. Katika kipindi hicho chote anastahili kupatiwa lishe
bora na maji ya kutosha ili akidhi mahitaji ya ndani aliye tumboni na kutoa
maziwa mengi baada ya kuzaa.
17.4.1.Matunzo ya ng’ombe mwenye mimba.
Mambo ya kuzingatia ni pamoja na
Ø Ng’ombe apewe lishe bora na maji ya
kutosha kipindi chote cha mimba
Ø Miezi 2 kabla ya kuzaa apewe kilo 2
za chakula cha ziada kwa siku
Ø Apewe kinga dhidi ya maambukizi na
tiba ya magonjwa
Ø Ng’ombe anayekaribia kuzaa, hususani
mtamba, azoeshwe kuingia kwenye sehemu ya kukamulia.
17.5.0.Dalili za ng’ombe anayekaribia kuzaa
Mfugaji anapaswa kufahamu dalili za
ng’ombe anayekaribia kuzaa ili aweze kufanya maandalizi muhimu.
17.5.1.Dalili
zake.
Dalili hizo ni pamoja na
1) Kujitenda kutoka kwa wenzake
2) Kiwele kuongezeka
3) Chuchu kutoa maziwa zikikamuliwa
4) Kutokwa na ute mwekundu na sehemu za
uke kuvimba na kulegea
5) Kuhangaika kulala chini na kusimama
na

17.6.0.Huduma kwa ng’ombe anayezaa.
Ng’ombe anayezaa anahitaji uangalizi
wa karibu ili kuhakikisha usalama wa ng’ombe na ndama anaezaliwa.
17.6.1.Mambo ya kuzingatia kwa huduma za ng’ombe anaezaa.
Mambo ya kuzingatia ni pamoja
na yafuatayo:-
a) Sehemu ya kuzalia ng’ombe iandaliwe
kwa kuwekwa nyasi kavu na laini na iwe safi.
b) Ng’ombe ahamishwe sehemu
iliyoandaliwa kwa ajili ya kuzaa mara baada ya dalili za kuzaa kuonekana
c) Ng’ombe aachwe azae mwenyewe bifa
usumbufu
17.6.2.Maswala ambayo mkulima anahitaji msaada wa kitaalamu.
Mfugaji apate ushauri/huduma kutoka
kwa mtaalam iwapo matatizo yafuatayo yatajitokeza:-
v Ng’ombe kushindwa kuzaa kwa masaa
mawili hadi matatu baada ya chupa kupasuka
v Kondo la nyuma kushindwa kutoka
masaa sita baada ya kuzaa
v Kizazi kutoka nje na
v Ng’ombe kushindwa kusimama baada ya
kuzaa
17.6.0.Matunzo ya ng’ombe anayekamuliwa.
Ng’ombe anayekamuliwa anahitaji
kupata chakula kwa ajili ya kujikimu na cha ziada kwa ajili ya uzalishaji wa
maziwa. Ili kukidhi mahitaji ya uzalishaji wa maziwa ng’ombe:
a) Apewe chakula cha ziada kwa kiwango
cha kilo 1 kwa kila lita 2 – 3 za maziwa anayotoa.
b) Apewe madini na virutubisho vingine
kulingan ana mahitaji
c) Apewe maji mengi kwa vile ni ya
muhimu katika kutengeneza maziwa.
d) Aachwe kukamuliwa siku 60 kabla ya
kuzaa. Uachishwaji huu ufanywe taratibu ili ifikapo siku ya 60 kabla
ya kuzaa ukamuaji usitishwe.
e) Baada ya kusitisha kukamuliwa apewe
kilo 2 za chakula cha ziada kwa siku hadi atakapozaa na
f) Apatiwe kinga dhidi ya maambukizi ya
magonjwa na tiba kulingana na ushauri wa mtaalam wa mifugo.
17.7.0.Uzalishaji wa maziwa.
Lengo la ufugaji wa ng’ombe wa
maziwa ni kupata maziwa mengi, safi na salama pamoja na mazao yatokanayo na
maziwa .
Mambo muhimu ya kuzingatia ni:-
Ø Sehemu ya kukamulia iwe safi na
yenye utulivu
Ø Ng’ombe awe na afya nzuri msafi na
kiwele kioshwe kwa maji safi ya uvuguvugu.
Ø Mkamuaji awe msafi kucha
fupi na asiwe na magonjwa ya kuambukiza
Ø Inashauriwa mkamuaji
asibadilishwebadilishwe
Ø Vyombo vya kukamulia viwe safi
Ø Muda wa kukamua usibadilishwe.
Ø Maziwa ya mwanzo kutoka kila chuchu
yakamuliwe kwenye chombo maalum (strip cup) ili kuchunguza ugonjwa wa kiwele.
17.8.0. Uchaguzi wa utunzaji wa dume bora la mbegu.
Dume ndilo linalojenga ubora wa
kundi la ng’ombe katika masuala ya uzalishaji kutokana na uwezo wake
wa kupanda majike 20 – 25 wakati wa msimu wa uzalianaji (breeding season).
Ili kundi la ng’ombe liwe bora,
mambo yafuatayo yazingatiwe
1) Chagua dume kutoka kwenye ukoo ulio
bora kwa kuzingatia kumbukubu za uzalishaji wa maziwa au nyama za wazazi wake.
2) Mfugaji apate ushauri wa mtaalam wa
mifugo katika kuchagua dume bora
3) Lisha dume malisho bora na maji safi
ya kutosha. Pia apatiwe chakula cha ziada.
4) Katika ufugaji shadidi dume la
ng’ombe lifugwe kwenye banda imara lenye sehemu za kuwekea chakula
maji na kufanyia mazoezi.
5) Katika ufugaji huria dume atengewe
sehemu na kupatiwa chakula cha ziada.
6) Dume livalishwe pete puani kwa ajili
ya kupunguza ukali na kuwezesha urahisi wa kumshika.
7) Dume apatiwe kinga na tiba ya
magonjwa kulingan ana ushauri wa mtaalam wa mifugo na
8) Mfugaji apate ushauri wa mtaalam wa
mifugo katika kuchagua dume bora.
18.0. UDHIBITI WA MAGONJWA YA NG’OMBE.
Magonjwa huweza kusababishwa na
matunzo hafifu lishe duni na visababishi vya magonjwa kama vile protozoa
bacteria.
Virusi, riketsia na minyoo. Aidha
wadudu kama kupe na mbung’o wanasambaza visababishi vya magonjwa.
18.1.0. Afya bora ya ng’ombe.
Afya bora ya ng’ombe inatokana na
kuzingatia mambo yafuatayo:-
v Ndama apate maziwa ya awali (dang’a)
ya kutosha kwa siku 3 – 4 baada ya kuzaliwa ili kuongeza kinga ya magonjwa
mwilini.
v Chovya kitovu cha ndama ndani ya
madini joto (Tincture of Iodine) mara baada ya kuzaliwa kuzuia kuvimba kitovu
kutokauka au kutohudumiwa ipasavyo mara baada ya ndama
kuzaliwa. Kitovu huvimba na kutoa usaha hukojoakwa shida na wakati
mwingine huvimba viungo.
v Ndama apewe dawa ya kuzuia minyoo
kila baada ya miezi 3 kama atakavyoshauri mtaalam wa mifugo. Minyoo
huwashambulia ndama zaidi hasa wale walioana kula majani.
v Zingatia usafi wa vyombo na band a
epuka kumpa ndama maziwa yaliyopoa na machafu ili kuzuia kuharisha.
v Zingatia ujenzi wa mabanda kuruhusu
mzunguko wa hewa ili kuzuia ndama kupata ugonjwa wa vichomi. Vichomi
huwapata ndama wa umri wa miezi 5 au zaidi wanaofugwa ndani katika mabanda
machafu yasiyo na mzunguko wa hewa ya kutosha.
v Ogesha ng’ombe kulingana na ushauri
wa mtaalam wa mifugo ili kuua kupe wote wanaoleta magonjwa yatokana yo na kupe
(ndigana kali na baridi, kukojoa damu na maji moyo) na mbung’o (ndorobo) na
v Ng’ombe wapatiwe chanjo dhidi ya
magonjwa mbalimbali chanjo muhimu ni za ugonjwa wa kutupa mimba, kimeta,
ugonjwa wa miguu na midomo na chambavu.
18.2.0.Msaada wa kitaalamu.
Mfugaji anashauriwa kutoa taarifa
kwa mtaalam wa mifugo anapoona ng’ombe wake ana baadhi ya dalili zifuatazo:-
Ø Joto kali la mwili na manyonya
kusimama
Ø Amepunguza hamu ya kula
Ø Amezubaa na kutoa machozi
Ø Anasimama kwa shind ana kusinzia
Ø Anapumua kwa shida na pua kukauka
Ø Anatokwa na kamasi nyingi
Ø Anajitenga na kundi
Ø Anaconda na
Ø Anapunguza utoaji wa maziwa ghafla
18.3.0.Dalili za magonjwa na toba.
Kwa dalili za magojwa na tiba
zake,tafadhli rejea kipengele cha magonjwa
yanayoenezwa na kupe kwa ng’ombe wa asili,kwani magojwa hayo huingiliana.
19.0.KUMBUKUMBU NA TAKWIMU MUHIMU
Kumbukumbu ni taarifa au maelezo
sahihi yaliyoandikwa kuhusu matukio muhimu ya kila ng’ombe na shughuli zote
zinazohusiana na ufugaji. Mfugaji anashauriwa kuweka kumbukumbu na
takwimu muhimu katika shughuli zake za ufugaji wa
ng’ombe. Kumbukumbu zinamsaidia mfugaji kujua mapato na matumizi na
kufanya maamuzi sahihi kuhusu mifugo husika na mifugo husika na mazao
yake. Aidha humwezesha kuweka mipango ya shughuli zake.
Mfugaji anapaswa kuweka
kumbukumbu muhimu zifuatazo:-
Uzazi (uhimilishaji na matumizi ya
dume, tarehe ya kupandwa, kuzaa kuachisha kunyonya)
v Kinga na tiba
v Utoaji wa maziwa
v Ukuaji
I like it
ReplyDeletendama wa kike anatakiwa afike umri gani ndo apandwe ...na nikitaka dume 1 ambaye ni mbegu nzuri na jike moja mbegu nzuri inaweza kuwa kiasi gani
ReplyDeleteAsante sana kwa elimu hii
ReplyDeleteIli nipate ndama jike nifanyeje?
ReplyDelete