Tuesday 17 April 2018

KWANINI NI MUHIMU KWAKO KUTUMIA TUNDA LA PARACHICHI KILA SIKU.


FAIDA ZA TUNDA

1. Vitamini A-iliyo kwenye parachichi inauwezo mkubwa kuimalisha uwezo wa macho na kuimalisha kinga ya mwili na hivyo kuwa mbali na magonjwa.

2. Ni tunda lenye kiasi kikubwa cha vitamin B:kuanzia B1,B2,B3,B6,B9 na B12  ambayo ni mhimu sana kwa mfumo wa misuli ya mwili na mifumo ya fahamu na kuweza kusaidia kuepuka na matatizo ya kupooza na  matatizo mengine ya nerve

3. Vitamini C- iliyo kwenye parachichi husaidia sana upande wa kuimarisha ngozi na kuifanya ngozi kuwa yenye kung’aa na kupendeza.

5. vitamini E (Alpha-tocopherol)
– husaidia kuzuia kuharibiwa kwa seli za mwili na kuzifanya kutozeeka kwa haraka pia huweza kusaidia kuimarisha seli za uzazi,na hivyo kuongeza nguvu za kiume.

6. vitamini K- huweza kuzuia damu zaidi kutoka kwenye jeraha kwa kuigandisha,kusaidia katika utengenezaji wa seli nyekundu za damu,pia husaidia usafirishaji wa madini ya kalsiamu na kuweza kuzuia uharibifu wa mifupa.
7.husaidia kuepusha na magonjwa ya moyo.

Madini ndani ya parachichi.

1. Parachichi lina kiasi kikubwa cha  madini ya Chuma  ambayo ni mhimu kwa utengenezaji wa seli nyekundu za damu (haem group) ambayo ndio husafirisha katika mwili wa binadamu.
1.      Madini mengine ni pamoja na kalsium n.k
ANZA KULA TUNDA HILI LENYE UMHIMU MKUBWA KATIKA MWILI WAKO LEO.

No comments:

Post a Comment