Tuesday 1 May 2018

KUKU WA AJABU NA GHARI ZAIDI DUNIANI.


Tumezoea kuona kuku aina ya kuchi akiwa ndo kuku anayeongoza kwa bei katika maeneo mengi ya Tanzania hata duniani kwa ujumla.Huko nchini Indonesia,Ulaya na marekani, kuku aina ya Ayam Ceman ndio ametokea kuwa ndo kuku wa ajabu na wa ghari zaidi duniani,ambapo huuzwa kati ya US $ 100-2500, sawa na pesa taslimu za kitanzania kati ya ~laki mbili na ishirini mpaka milioni tano na nusu(221500-5537500).
ASILI YA JINA  AYAM CEMANI.
Neno Ayam  humaanisha kuku kwa lugha ya huko Indonesia na Cemani ni kijiji kwenye kisiwa cha Java ambako ndio kuku hao wametokea.
ASILI YAO.
Kuku hawa wanaasili ya Indonesia katika visiwa vya Java.kuku hawa kwa sasa hawapatikani maeneo mengi duniani,ambapo ulaya kwa mara ya kwanza walifikishwa na mtaalamu wa uzalishaji wa mbegu za kuku Bwana Jan Steverink mwaka 1998.
JINSI WALIVYO.
Ayam Cemani ni kuku wa kushangaza kidogo kwani kila kitu cha mwili wao ni cheusi kuanzia manyoya,midomo,ulimi,nyama yao na hata mifupa yao isipokuwa  mayai yao huelekea kwanye pinki,pia viungo vingine vya ndani kama filigisi maini n.k huwa ni meusi tii na hiyo yote ni kwa sababu ya uwingi wa melanini katika miili yao na hali hii kitaalamu hufahamika kama fibromelanosis. kuku hawa wa ajabu huwa na uzito wa kilo 2-2.5 kwa majogoo na kilo 1.5-kilo 2 kwa mitetea kama ilivyo kwa kuku wengi wa kisasa kuku hawa ni nadra kuatamia mayai yao.
Picha zote ni kwa hisani ya google.com/
Kuku mwenyewe.
ndani ya mdomo.
 
Nyama yao.

Kwanini wauzwe pesa nyingi kiasi hiki?
Zipo nadharia kadhaa juu ya ughali wa kuku hawa moja wapo ikiwa ni kutumika kwake kwa masuala ya kiimani na kuna kila uwezekano kwamba kuku hawa kwa miaka mingi huko Indonesia wamekuwa wakitumika kwenye ibada za miungu na ya pili ni kutumia kama mapambo katika eneo ampapo anafugwa.

No comments:

Post a Comment