Moja ya sababu za kuitwa matunda yenye umhimu na ubora zaidi zina ainishwa katika machapisho yetu hapa.
Vitamin A (beta-carotene) iliyo kwenye papai ni nyingi mara tatu ya ile iliyo kenye karoti na nyanya.hivyo mtu anayekula papai ana faida ya kupata vitamin A mara tatu kuliko ya yule anayetumia karoti na nyanya.
Utafiti uliofanywa na kuchapishwa na jarida la afya la uingereza la British Journal of Nutrion(British Journal of Nutrition) utafiti ambao uliwashirikisha watu 16 ambao walipewa kula karoti,nyanya na papai ambapo matokeo yake ni papai lilikuwa bora sana.
Kikombe kimoja cha juice ya papai ina kiwango kikubwa cha vitamin c kuliko kikombe kama hicho cha chungwa hii ina maana kuwa papai lina vitamin c nyingi kuliko chungwa.
Virutubisho vingine ambavyo papai linalo ni pamoja na flavonoids; vitamin B,, foleti na pantotheniki asidi; Madini kama, potassium, copper, magnesium; na pamoja na nyuzinyuzi kiasi kidogo.
KAMA HUPENDELEI KULA MAPAPAI BASI JUA KUA UNAKOSA VIRUTUBISHO VINGI, HIVYO ANZA LEO.
No comments:
Post a Comment